Kocha wa timu ya Chelsea, Thomas Tuchel ameeleza kuwa wachezaji wake wawili wa kikosi cha kwanza Mateo Kovacic na beki wake Andres Christensen watakosa mchezo wa leo wa EPL dhidi ya Arsenal kutokana na majeraha waliyopata katika mechi iliyopita.

Chelsea watawaalika washika bunduki Arsenal pale Stamford bridge katika mbio za kuwania kucheza ligi ya mabingwa ulaya msimu ujao. Arsenal pia wanapambana ili kuweza kupata alama tatu za kuwasogeza  kwenye Top 4.

Kabla ya ujio wa Thomas Tuchel Chelsea ilikuwa katika kipindi kibaya sana na haikuonekana kuwa tishio licha ya usajili mkubwa uliofanya. Lakini Tuchel amerejesha matumaini makubwa kwa wana Blues na huenda huu ukawa ni msimu wa mafanikio sana kwao kwani wanaweza kutwaa makombe mawili, FA Cup na UEFA Cup.

Vijana hawa wa Tuchel watacheza na Leicester City wikiendi hii kuwania kuchukua kombe la FA na mwisho wa mwezi huu watakutana na mabingwa wa EPL, Man City katika fainali ya ligi ya mabingwa ulaya. 

Kocha huyo wa The Blues alisema, “Kova hayupo tayari kwa mechi ya kesho (leo). Malengo ya kumtumia huyu yapo katika mchezo wa Wembley. Andres nae anaonekana kuwa vizuri lakini tunahofia kumuanzisha kesho, tuna michezo miwili dhidi ya Leicester City na uwepo wake ni muhimu.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Tuchel, Tuchel Ataja 2 Watakaowakosa Arsenal Leo, Meridianbet

CHEZA HAPA

6 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa