Tuchel Bado Anaipenda Chelsea

Kocha wa klabu ya Bayern Munich ambaye amewahi kuifundisha klabu ya Chelsea Thomas Tuchel ameonesha wazi mahaba yake juu ya klabu yake hiyo ya zamani aliyoitumikia kwa mafanikio.

Tuchel alipoulizwa juu ya yeye kurejea kwenye ligi kuu ya Uingereza baada ya kuachana na klabu ya Bayern Munich na kusema “Siwezi kujibu hili lakini sio siri nilipenda maisha ya Chelsea,Uingereza, na Ligi kuu ya Uingereza ulikua wakati mzuri sana ndani ya Uingereza”tuchelKocha huyo wa zamani wa klabu ya Chelsea inafahamika kua mwishoni mwa msimu huu atatimka ndani ya klabu ya Bayern Munich baada ya kudumu kwa muda wa mwaka mmoja na nusu klabuni hapo, Lakini matokeo yake hayakua ya kuvutia na klabu hiyo kuamua kuachana nae kufikia mwisho wa msimu huu.

Kocha huyo wa kimataifa wa Ujerumani ameonesha wazi kua bado anavutiwa na klabu ya Chelsea na maisha ya Uingereza kwa ujumla, Jambo ambalo linatafsiriwa kua anaweza kurejea ndani ya klabu ya Chelsea mbeleni kutokana mwenendo wa klabu hiyo.tuchel

Mbali na klabu ya Chelsea lakini kocha huyo amekua akihusishwa na vilabu kadhaa kutoka nchini Uingereza vikihitaji huduma yake, Huku klabu ya Manchester United ikiwa ni miongoni mwa vilabu vinavyotajwa sana kuwania saini ya kocha Tuchel ambaye ataondoka ndani ya Bayern Munich mwishoni mwa msimu huu.

Acha ujumbe