Meneja wa Chelsea, Thomas Tuchel anaamini kuwa kinda wa klabu hiyo, Conor Gallagher yuko tayari kuwa sehemu ya kikosi chake pale Stamford Bridge msimu ujao.

Gallagher, 22, ambaye amekuwa kwenye kiwango bora msimu huu anaitumikia Crystal Palace kwa msimu mzima akitokea katika klabu yake ya Chelsea.

 

tuchel, Tuchel : Gallagher Atarejea Msimu Ujao., Meridianbet

Kiungo huyo wa kati wa box-to-box amekuwa mchezaji muhimu kwa Crystal Palace, akifunga mabao nane na kutoa pasi tano za mabao katika michuano yote msimu huu.

Tuchel amekuwa akimjadili Gallagher kwa undani kabla ya Kombe la FA. Akidai anamwona kama mchezaji anayeweza kucheza katika kikosi cha kwanza cha Blues msimu ujao atakaporejea.

“Ninaamini kwamba Conor anaweza kuwa sehemu ya kikosi chetu na anaweza kucheza na sisi lakini sio mimi pekee ninayeweza kuamua,” Tuchel alisema.

 

“Tunahitaji kuzungumza baada ya msimu na kila mtu na tunahitaji kuona kile Conor anataka. Tunahitaji kuona hali ikoje, tuna nafasi gani kwake na nini anaweza kupigania kwa sababu unahitaji kitu cha kupigania.” aliongeza.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa