Neymar amerejea vyema katika mechi yake ya kwanza ya msimu akiwasaidia PSG kupata ushindi wa 1- 0 dhidi ya Strasbourg Jumamosi.
Wakati wa mechi hii Neymar alilengwa na mashabiki waliokuwa wanamzomea kufuatia minong’ono kuwa alikuwa anaishinikiza klabu kukamilisha uhamisho wake kwenda Barcelona.
Kocha wa PSG, Tuchel anasema staa huyu hana namna zaidi ya kukubali kuzomewa na mashabiki, na alipenda namna Neymar alivyolipokea suala hilo bila jazba.
Hata hivyo, Neymar aliwaziba mdomo mashabiki waliomzomea kwa goli alilofunga dakika ya 90 ya mchezo, goli pekee lilioipa klabu yake ushindi.
“Haikuwa rahisi, ni mtu mwenye hisisa sana, lakini alifanya vyema.” Tuchel akimzungumzia Neymar. Pia alisisitiza kuwa haikuwa rahisi pia kwa upande wa mashabiki kwa stori walizokuwa wanazisikia wakati wa dirisha la usajili na hakuna budi kuikubali tabia wanayoionesha.
Baada ya ushindi wa Jumamosi, PSG wanabakia kwenye nafsai ya kwanza kwenye Ligue 1 baada ya kushinda mechi yao ya 4 kati ya tano walizocheza msimu huu.
Povel
Neymar fundiiii