Meneja wa Chelsea, Thomas Tuchel amewapongeza wachezaji wake kwa kujituma katika mchezo wa jana ukiachana na kuambulia alama moja nyumbani dhidi ya Manchester United.

Tuchel amesema kuwa pointi moja waliyopata mbele ya Manchester United, uwanjani Stamford Bridge si haba kwa kuwa wachezaji walipambana kusaka ushindi.

 

tuchel, Tuchel : Wachezaji Wanastahili Pongezi., Meridianbet

Mchezo huo uliochezwa usiku wa kuamkia leo ulikuwa na ushindani mkubwa huku utata wa penati na VAR ukizidi kuongeza mvuto wa mechi hiyo iliyokuwa na kasi kwa dakika zote 90.

Manchester United wakilalamika kwamba walinyimwa penalti ya wazi kwenye mchezo huo uliokamika ubao kusoma 0-0.

Penalti hiyo ambayo VAR iliikataa na kumfanya mwamuzi wa kati Stuart Attwell kuifuta ilionekana nyota wa Chelsea Callum Hudson-Odoi akiugusa mpira huo walipokuwa wakipambana na Mason Greenwod na uliwagusa wote wawili kwenye mikono walipokuwa ndani ya 18.

Matokeo hayo yanaifanya Chelsea kufikisha jumla ya pointi 44 ikiwa nafasi ya 5 huku United ikibaki nafasi ya pili na pointi 50. Kinara ni Manchester City mwenye pointi 62.


Ni Muda wa Kuvuna Mkwanja na Jungle Jim and the Lost Sphinx

Huhitaji kufikiria mara mbili ni mchezo gani utakupatia mkwanja ndani ya kasino za Meridianbet. Jiunge sasa ufurahie Jungle Jim and the Lost Sphinx.

tuchel, Tuchel : Wachezaji Wanastahili Pongezi., Meridianbet

  CHEZA HAPA

7 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa