Kombe la mataifa ya Afrika ambalo ndilo linajulikana kama AFCON ni kati ya mataji makubwa sana kwenye soka la Afrika na lina heshima ya pekee sana kwa kukutanisha wachezaji wa mataifa mbalimbali wakiwa katika hali za kulinda na kutetea heshima za nchi zao na kuwapa mashabiki zao wanachokitaka.
Mashindano yake huratibiwa chini ya shirikisho linalojulikana kama Confederation of African Football [CAF] ambalo linatambulika kisheria na FIFA kwa misingi yote ya usimamizi na udhibiti wa mashindano hayo ndani ya bara zima la Afrika na kila kinachotendeka hufuata misingi ya kisheria ya Shirikisho la Soka Duniani.
Kwa mara ya kwanza lilichezwa mwaka 1957 kukiwa na mataifa kama Egypt, Sudan, South Africa na Ethiopia ambao walitengeneza ushindani ndani ya kombe hilo kwa kipindi hicho. Lakini kabla ya mkutano wa wanachama hao huko Lisbon mwaka 1956 kulikuwa na baadhi ya maafikiano ambayo yalifanyika.
Mwaka 1957 mashindano yalifanyika huko Khartoum, Sudan wakati huo Afrika ya Kusini kukiwa na ubaguzi wa rangi mkubwa sana kitu ambacho kilipelekea kuchaguliwa kwa wachezaji wenye asili ya nje pekee ndani ya kikosi, jambo lililopelekea kutemwa kama adhabu na kumpa Ethiopia nafasi ya wazi kuingia kucheza fainali na Misri.
Katika fainali hiyo, Misri waliibuka mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo mikubwa. Hapo ndipo utawala wa Misri kwenye kombe hilo ulipoanza, wakawa ni mabingwa wa kihistoria sana ndani ya Afrika nzima. Ambapo pia hata mara ya pili walipopata nafasi ya kuandaa kombe hilo walishinda tena.
Mwaka 1962 ilishuhudiwa pande ambazo zilikuwa zikitaka kushiriki kombe hilo; ambapo waliweza kutengeneza jumla ya mataifa sita yaliyopata nafasi ya kuongezeka kwenye ushiriki huo. Mataifa kama Nigeria na Tunisia yalikuwa sehemu ya ongezeko hilo nje ya yale manne yaliyokuwa wanachama wa mapema kabisa.
Kuanzia hapo sasa mashindano yakawa makubwa sana na yenye heshima ya pekee kutoka timu tatu ambazo zilikuwa zinatinga hatua ya fainali mwaka 1958 na kufikia 24 mwaka 2019. Mbali na ile ya 1996 hadi 2017 ambapo timu 16 pekee zilikuwa zikipata nafasi ya kusonga hatua ya fainali kwenye michuano hiyo.
Mashindano ya mwaka huu ni ya 32 kihistoria na yatafanyikia huko Misri ambako ndiko historia ya mashindano hayo imejengeka kwa misingi mikubwa sana hadi hivi leo.
Ester jackson
Thanks meridian for news