Cristiano Ronaldo Hajawahi Kupenda Urahisi!

Cristiano Ronaldo amekuwa mshindi wa wakati wote kila anapoenda. Amekuwa akifanikiwa karibu kila hatua anayopiga katika soka.

Amekuwa somo kwa wanasoka wachanga na nje ya soka kwa kujituma kwake. Abel Xavier anamtaja CR7 kama mtu asiyependa mteremko, anayependa kupiga kazi haswa.

“Popote anapoenda anaenda kushinda, peke yake na kama timu”

Sasa amerejea nyumbani. Safari ya Cristiano Ronaldo haijawa safari ya matumaini, bali safari ya ushindi katika kila timu na ligi aliyoshiriki. Akiwa kijana tu, akiungana na Manchester United, Ronaldo alikuwa chachu ya ushindi wa timu na kushinda tuzo binafsi katika ulimwengu wa soka.

Katika miaka yake 6 ya awali akiwa na Manchester United, alishinda mataji 3 ya ligi, makombe mawili ya EFL, FA Cup, na Ligi ya Mabingwa mwaka 2008.

'Ronaldo Hajawahi Kupenda Mteremko
Ronaldo -Man United

Safari yake ya neema alienda nayo Real Madrid. Ambako katika kipidndi chake cha miaka 9, amekuwa akiongoza kwa magoli klabuni hapo. Ameshinda mataji mawili ya LaLiga, mataji mawili ya Copa del Rey, na mataji manne ya Ligi ya Mabingwa.

'Ronaldo Hajawahi Kupenda Mteremko
Ronaldo -Madrid

Safari yake haijaishia hapo. Aliamua kuondoka Madrid kuelekea Juventus kuelekea msimu wa 2018/19. Katika msimu wake wa awali tu ameweza kushinda Serie A na Supercoppa Italiana.

cristiano ronaldo manchester-united
Cristiano Ronaldo amerejea na kuanza vyema msimu kwa kuchapa magoli 2 ya ligi, na goli moja ligi ya mabingwa.

Huyu ndiye Cristiano Ronaldo. Mafanikio yake, ukiacha mbali kuwa na kipaji yanachochewa na namna anavyojituma. Abel Xavier, ambaye amewahi kushirikiana na Ronaldo katika kikosi cha Ureno anasema CR7 ni mchapa kazi.

“[Ronaldo] Ni mshindi na uzingatiaji wake ni mkubwa sana. Unaweza kuona siyo mtu amabaye anapenda urahisi. Alikuwa Madrid, akashinda; Alikuwa Man United, alishinda, Real Madrid alishinda, Juventus nako alipata mafanikio, bila kusahau mafanikio yake na timu ya taifa.

CR7 amekuwa somo la kusomwa na kila mtu anayependa kufanikiwa. Kujituma ni nguzo ya mafanikio. Heshima, busara na kuishi vizuri na watu wengi. Kwa pamoja haya ni ufunguo wa mafanikio, vitu ambavyo uwe mwanasoka au si mwansoka unaweza kujifunza kutoka kwake.


MKWANJA NJE NJE NA DISCO FUNK

Unaanzaje siku yako na kuimaliza bila kupitia katika kasino bomba za meridianbettz, mchezo mashuhuri wa Disco Funk unaweza kukufanya uwe mshindi leo hii.!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe