Guardiola: Hatujali Kabisa!

Kocha wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola alisema kwamba hatojali lolote lile endapo kikosi chake kingemaliza msimu bila kuwa na taji lolote. Kocha huyo ametasema hayo kwa kuona kwamba hana wasiwasi wa namna ambavyo wengi wanahisi hatakuwa na amani kunyanyua kikombe ndani ya msimu huu kutokana na kuwa na matokeo mabovu ambayo hayaendani kabisa na kasi yake ya msimu uliopita.

Kocha huyo aliona kwamba hadi sasa mataji ambayo aneyanyanyua mfukulizo na klabu hiyo ni kipomo tosha kabisa cha kuweza kuaminisha kwamba anaweza kazi yake hiyo. Amenyanyua kombe la ligi mara mbili mfululizo akiwa na kikosi hicho na makombe mengine ya ndani. Kwa hiyo suala hilo halimpi wasiwasi.

Ramani hiyo imeanza kuonekana mara baada ya kocha huyo kuona kwamba watu wameanza kumwangalia kwa namna nyingine kutokana na kupoteza mechi yake mbele ya klabu iliyopanda ligi msimu huu pia mara baada ya kuwa na mwenendo ambao kikosi chake kinaonesha kusuasua sana ndani ya ligi hiyo.

Maajabu ambayo hayatasahaulika kwa kocha huyo ni kunyanyua kombe akiwa na alama nyingi sana katika ligi ambazo zilikuwa 98 jambo ambalo kwa miaka ya karibu lilikuwa kama historia na mapinduzi makubwa katika soka la Uingereza. Hivyo, kwake hilo sio changamoto na aliliona halina nguvu kumpa mawazo sana.

Jimgine ambalo kocha huyo alijaribu kulizungumzia ni juu ya hali halisi ilivyo kikosini hapo kwa sasa kwamba sio rahisi sana kutokana na kuanza msimu kwa kuwa na wachezaji ambao ni majeruhi, tena wachezaji ambao ni muhimu sana katika kikosi chake cha kwanza; hivyo hilo ni jambo ambalo kwake bado ni changamoto kiasi fulani.

Akiwa kama kocha pia amezungumzia suala la kuwa na wach3zaji wa aina moja katika misimu kadhaa mfululizo kwamba nalo huwa linashusha ushindani kwa sababu kikosi hicho huwa tayari kimeshinda kila kitu na kuona kwamba ni hali ya kwaida sana hata pale wanapotokea kukosa ubingwa fulani.

Lakini mbali na hilo ametahadharisha kwamba hilo sio sababu ya yeye kukata gamaa ya kufukuzia ubingwa bali ni onyo tu la kawaida ambalo ameliweka kwa wale wanaoona kwamba kocha huyo huenda ameanza kukubali hali halisi ya ligi kwa msimu huu. Kwamba atashindwa kufanya vyema kabisa.

40 Komentara

  man saiv amna kitu wabovu

  Jibu

  Kocha wa Manchester city
  Anajitahidi Sana japokuwa anipitia
  Changamoto

  Jibu

  Man u wameshaishiwa

  Jibu

  Ni ulemsemo wa sizitaki mbichi hizo Pep anautumia apo

  Jibu

  Kwa uwekezaji mkubwa kama wacity alafu kumaliza msimu bila kombe lolote!!!

  Jibu

  Pep ni jasiri sana

  Jibu

  Pep ni kocha bora

  Jibu

  kashaishiwa uyo Hana lolote

  Jibu

  Anajibaraguza huyo

  Jibu

  Huyu ni aina ya makocha wanaojua nini wanafanya …

  Jibu

  Anajipa moyo tu,uku kiroho kinauma

  Jibu

  Anatakiwa asifanye ivo ,apambane ili wafikie malengo.

  Jibu

  hiyo ni kocha anayejua#meridianbettz

  Jibu

  Guardiola yuko vizuri anajikubali sana na ndio maana hajali chochote kile

  Jibu

  Hana jipya anajishitukia tu huyo anarapu tu hapo ila moyoni kunaongea vingine

  Jibu

  Kila mtu anamapungufu yake ila Guardiaola aliweza fanya Mambo mazuri tu

  Jibu

  Pep bado ni kocha bora kwa upande wangu

  Jibu

  Shuhul mnayo watu wa man

  Jibu

  Pepe kwa upande wake yuko sahihi kabisa ila mashabiki watahitaji waone man city inachukua taji

  Jibu

  Big coach pep namkubali Sana! Safari hii Liverpool anastahili tumpe ubingwa wake.#meridianbettz

  Jibu

  Kocha pep Guadiola ni kocha anayejiamini anaamini yeye si mtu wa kushindwa hii iko poa sana

  Jibu

  Guadiola ni kocha mwenye upeo mkubwa anajua n Nini anafanya

  Jibu

  Guardiola unazingua maneno gan ayo ya kutatsha tamaa wachezaj na mashabiki

  Jibu

  Man hawana jipya..

  Jibu

  hilo sio sababu ya yeye kukata tamaa ya kufukuzia ubingwa #meridianbettz

  Jibu

  tena wachezaji ambao ni muhimu sana katika kikosi chake cha kwanza; hivyo hilo ni jambo ambalo kwake bado ni changamoto kiasi fulani. #meridianbet

  Jibu

  Pep ni moja Kati ya makocha Bora dunia kwa Sasa thnks meridian kwa update za michezo

  Jibu

  Pep ni jasiri sana napia ni kocha nzur sana

  Jibu

  Pep bado Yuko vzr

  Jibu

  Ashawachoka sana

  Jibu

  Mbinu zishaisha Hana Tena ujanja inabidi akubali matoke

  Jibu

  Hatutaki maneno si tunataka vitendo mashabiki

  Jibu

  Gadiola sijaipenda maneno yako

  Jibu

  huyu pep anajifariji tu anyway mwache ajidanganye maboss zake ni watu wa maamuzi ya haraka

  Jibu

  Pep yupo vizuri

  Jibu

  Man ilikuwa zamani bhanaa

  Jibu

  Gadiola uwenda kunaacho jivunia

  Jibu

  Ni kocha mzuri Sana na anatambua anachokifanya

  Jibu

  Pep ni kocha bora

  Jibu

  Guardiola ni kocha mahiri asiyenamfanoe kwa sasa hapa duniani #meridianbettz

  Jibu

Acha ujumbe