Shirikisho la Soka la Tunisia lilimtimua kocha wa timu ya taifa, Mondher Kebaier kufuatia kushindwa kufuzu robo fainali katika Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2021.
Tunisia imethibitisha kumfukuza kocha Mondher Kebaier baada ya timu hiyo kushindwa kufuzu kwa robo fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Cameroon.
Safari ya The Eagles of Carthage kwenye mashindano ya 33 ilikamilika katika hatua ya nane bora baada ya kupoteza 1-0 dhidi ya wachezaji 10 Burkina Faso kwenye Uwanja wa Omnisports Roumde mjini Garoua, Jumamosi.
Tunisia wamefichua katika taarifa kwamba wameachana na Kebaier, na nafasi yake itachukuliwa na msaidizi wake Jalal Al-Qadri.
“Iliamuliwa kusitisha uhusiano wa kimkataba na Mondher Kebaier na kumteua Jalal Al-Qadri kama mbadala wake,” Tunisia ilisema katika taarifa kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii.
“Tunamshukuru Mondher Kebaier kwa juhudi alizofanya katika kipindi alichokuwa akiinoa timu ya taifa, tukimtakia mafanikio katika maisha yake yote ya ukocha. Pia tunamtakia Jalal Al-Qadri mafanikio katika majukumu yake mapya.”
Meneja huyo mwenye umri wa miaka 51 alichukua mikoba ya Eagles of Carthage mnamo Agosti 2019, alipotia saini kandarasi ya miaka mitatu.
Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.