Tutaifunga Simba - Ibenge

Kocha mkuu wa AS Vita, Florent Ibenge amesema kuwa ili waweze kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika wanatakiwa kuibuka na ushindi katika michezo yao miwili iliyosalia ya ligi hiyo ikiwemo dhidi ya Simba.

AS Vita kwa sasa inashika nafasi ya 3 katika kundi A la ligi ya mabingwa mara baada ya kujikusanyia pointi 4 nyuma ya Simba waliona pointi 10 na Al Ahly ambao wamejikusanyia pointi saba.

Akizungumzia malengo yao katika michuano hiyo Ibenge amesema: “Tunatakiwa kushinda michezo yetu yote miwili iliyosalia dhidi ya Simba na Al Merrikh ili tuweze kusonga mbele katika hatua ya robo fainali.

“Matokeo tuliyopata hayajakuwa mazuri sana kwetu, lakini huu si muda wa kulaumiana tunachotakiwa kufanya ni kuhakikisha tunasonga mbele”.

AS Vita wanatarajia kucheza na Simba ugenini Aprili 2, katika Uwanja wa Mkapa, Dares Salaam huku mchezo wa mwisho ukitarajiwa kufanyika kwao nchini Congo April 9, wakicheza dhidi ya Al Merrikh.


Maana Kamili ya Ushindi Katika Kasino za Meridianbeti ni Pamoja na Mchezo wa Tropical Wild.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Tropical Wild na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

CHEZA HAPA

8 Komentara

    Sawaa

    Jibu

    Tunasubiri dakika90 tuone nani zaidi

    Jibu

    Duh kazi ipo

    Jibu

    Sawaa

    Jibu

    Acha tuone

    Jibu

    Tutaona

    Jibu

    Ibenge anajisumbua hawezi shinda kwa mkapa

    Jibu

    Wajipange tuuu

    Jibu

Acha ujumbe