Tyson Fury alionekana kumkejeli kwa utani juu ya majibu ya Anthony Joshua kwenye chapisho lake la mtandao wa kijamii, baada ya kupoteza pambano lake na Oleksandr Usyk.
Pambano hilo lilipiganwa Mjini Jeddah Jumamosi usiku, ambapo AJ alipigwa kwa pointi na mwana masumbwi huyo raia wa Ukraine kwa mara ya pili mfululizo na kushika vichwa vya habari kutokana na majibu yake baada ya pambano.
Wakati matokeo yalipothibitishwa, Joshua alijibu kwa hasira, akichukua mikanda miwili ya Usyk na kuitupa.
Kisha akajihusisha na majibizano ya hasira na baadhi ya washiriki wa Usyk na akatoka nje ya uringo. Kabla ya kurudi kwenye chumba chake cha kubadilishia nguo, ingawa, AJ alibadili mawazo na kurudi tena uringoni, kisha akachukua kipaza sauti na kutoa hotuba ya ajabu, lakini yenye kushangaza.
Fury aliingia kwenye mitandao ya kijamii na kukejeli hali hiyo huku akichapisha chapisho kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii.
Chapisho hilo lilionyesha kipande cha video cha Mfalme wa Gypsy akikimbilia ulingoni kwa pambano lake na Dillian Whyte, ambalo lilifanyika Aprili na kuandika: “AJ akirudi ulingoni kuzungumza takataka kabisa.”