Chelsea itashuka uwanjani kucheza dhidi ya Arsenal usiku wa leo, huu ukiwa mchezo wa 36 kwa Chelsea kwenye michuano hii ya Ligi Kuu Uingereza.

Arsenal

Mchezo huu ni wa muhimu kwa Chelsea katika harakati zake za kuwania nafasi nne za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Uingereza ambapo mpaka sasa Chelsea ina alama 64.

Aliye juu ya Chelsea ni Leicester city ambao wana alama 66 na chini ya Chelsea yupo West Ham mwenye alama 58.

Endapo Chelsea ikifanikiwa kupata ushindi dhidi ya Arsenal basi itakuwa imejihakikisha kumaliza ndani ya timu nne za juu kwa 90% maana itakuwa imefikisha alama 67, alama ambazo ili West Ham aifikie Chelsea atatakiwa kushinda michezo yote mitatu iliyosalia ili alingane alama na Chelsea.

chelsea
West Ham

Leicester kwasasa wana alama 66, alama ambazo wamezifikisha wakiwa wamecheza mchezo mmoja zaidi ya Chelsea, hivyo endapo Chelsea ikishinda mchezo wake dhidi ya Arsenal basi Chelsea itarejea kwenye nafasi ya tatu na itahitaji alama moja zaidi ili kujihakikishia nafasi kwenye nafasi nne za juu.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

arsenal, Uchambuzi: Chelsea Vs Arsenal, Meridianbet

CHEZA HAPA

12 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa