Uefa Champions League inarejea tena usiku wa leo na michezo kadhaa itapigwa katika viwanja tofauti tofauti yimu zikitafuta nafasi ya kufuzu katika hatua ya 16 katika ligi hiyo.

Michezo hiyo inapigwa ikiwa ni raundi ya tano ya michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya ikiwa timu zitabakiza mchezo mmoja ili kukamilisha michezo ya hatua za makundi ya michuano hiyo.uefa champions leagueChelsea watakua nchini Austria kupambana Rb Sarlzburg ili kujihakikishia nafasi ya kukaa kileleni mwa msimamo wa kundi E na kufuzu hatua ya 16 bora ya Uefa Champions league.

Real Madrid wao wamesafiri hadi nchini Ujerumani kukabiliana na Rb Leipzig Real madrid ambao wanaongoza kundi F tayari wameshajihakikishia nafasi ya kufuzu hatua inayofuata lakini watakua wanapambana kulinda rekodi yao ya kutopoteza mchezo wowote msimu huu mpaka wakati huu.uefa champions leagueKlabu ya Ac Milan watakua ugenini kukabiliana na Dinamo Zagreb, Milan ambao wanashika nafasi ya tatu kwenye kundi E watakua wanatafuta ushindi wao wqa pili kwenye kundi hilo baada ya kupoteza michezo miwili dhidi ya Chelsea hivo mchezo wa leo ni muhimu sana ili kutengeneza mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.Borussia Dortmund watakua nyumbani kuwakaribisha Manchester City ya nchini ya Uingereza katika mchezo wa kundi G huku klabu ya Dortmund ikitaka ushindi ili kujihakikishia kufuzu hatua inayofuata huku Manchester City wao wakiwa tayari wameshafuzu hatua inayofuata.

Mechi nyingine kali itakwenda kupigwa usiku wa leo itapigwa pale Ureno katika dimba la Estadio da Luz kati ya Benfica dhidi ya vibibi vizee vya Turin Juventus huku Juventus wao wakiwa na alama tatu pekee hivo watahitaji kushinda mchezo huu ili kusogea mbele zaidi na kuweza kufuzu hatua ya 16 bora.uefa champions leagueMichezo mingine itakayopigwa kwenye Uefa Champions league leo ni kati ya Shakhtar Donetsk dhidi ya Celtic, Sevilla dhidi ya Fc Copenhagen, na PSG wakiwa nyumbani kuwakaribisha Maccabi Haifa.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa