Kuelekea mchezo wa fainali ya Uefa 2021, bado hakijaeleweka kuhusu uwanja utakaotumika kwenye mchezo huo. Ureno yatajwa kwa mara nyingine mwaka huu.

Baada ya kufanyika mazungumzo kati ya Uefa, FA na serikali ya Uingereza. Bado hakujawa na makubaliano thabiti kwa pande zote na hivyo nchi mbadala zimeanza kuingia kwenye ramani ya mazungumzo mapya.

Licha ya Uefa kukubali kubadilisha uwanja kutoka nchini Uturuki na kuhamishia fainali nchini Uingereza (Wembley ikitajwa kama uwanja pekee uliopendekezwa) kutokana na changamoto za usafiri kati ya Uingereza na Uturuki, suala la kuondoa karantini kwa baadhi ya viongozi waandamizi wa mashindano hayo limekuwa ni gumu kwa serikali ya Uingereza.

Uefa, Uefa, Fainali Kuhamia Ureno? Hakieleweki., Meridianbet
Bayern Munich walitwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa msimu uliopita. Fainali ilichezwa jijini Lisbon, Ureno.

Kutokana na ugumu huo, Ureno ipo kwenye uwezekano wa kuandaa fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu huu. Itakumbukwa msimu uliopita, mji wa Lisbon ulitumika kwa michezo ya Ligi ya Mabingwa kuanzia hatua ya robo fainali mpaka fainali.

Endapo fainali ya Uefa itafanyika Ureno, itakuwa ni rahisi kwa vyombo vya habari, wadhamini na wadau wengine wa mashindano hayo kuhudhuria mchezo huo bila vikwazo vyovyote vya usafiri vinavyohusiana na COVID19. Hii itakuwa ni bahati kwa Ureno kuandaa michezo ya Ligi ya Mabingwa kwa miaka miwili mfululizo.

Manchester City na Chelsea zinasubiri tamko kuhusu uwanja watakaochuana kupambania ubingwa wa Uefa msimu huu. Timu zote zinatarajia kupewa tiketi 4000 kila mmoja ili mashabiki wa timu hizi waweze kuhudhuria mchezo huo.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Uefa, Uefa, Fainali Kuhamia Ureno? Hakieleweki., Meridianbet

CHEZA HAPA

7 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa