Kuelekea fainali ya Uefa, serikali ya Uingereza imepiga marufuku raia wa nchi hiyo kusafiri kwenda nchini Uturuki utakapochezwa mchezo wa fainali kati ya Man City vs Chelsea.

Mei 29,2021 mbivu na mbichi zitajulikana baada ya dakika 90 pale ambapo Pep Guardiola ataiongoza Man City kwenye mchezo wa fainali kwa mara ya kwanza kwenye historia ya klabu hiyo. Upande wa pili, Thomas Tuchel atakuwa ni kocha wa kwanza kuziongoza timu mbili tofauti kwenye hatua ya fainali kwa misimu miwili mfululizo, (PSG – 2020, Chelsea – 2021).

uefa

Katazo la serikali ya UK linakuja baada ya nchi hiyo kuiweka Uturuki kwenye orodha ya nchi zenye maambukizi makubwa ya COVID19 na hivyo kukataza wananchi wake kwenda nchini humo labda kuwa na sababu ya ulazima sana.

Katibu wa Usafiri wa nchini Uingereza, Grant Shapps ameongeza kuwa, FA ipo kwenye mazungumzo na Uefa kuhusu kubadilisha uwanja wa mchezo huo lakini huo ni uamuzi ambao upo kwa Uefa.”

Ungozi wa Ligi ya Mabingwa ulipanga kutoa jumla ya tiketi 4,000 kwa kila timu kwenye mchezo wa fainali utakaochezwa kwenye uwanja wa Ataturk Olympic.


TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

Uefa, Uefa: Hakuna Kwenda Uturuki, Imesema Serikali ya UK., Meridianbet

SOMA ZAIDI

8 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa