UEFA Kuamua ya Hazard…

Fununu zinazozidi kupasua anga juu ya uwezekano wa Hazard kujiunga na Madrid zinaendelea kuwa kichomi upande wa Chelsea wenyewe hasa kwa ngazi mbalimbali za uongozi wa klabu hiyo. Kinachotia vuguvugu hizo ni endapo Chelsea watakosa nafasi ya kushiriki UEFA msimu ujao itakuwa ni vigumu kwa nyota huyo kuendelea kuwepo hapo.

Eden Hazard huenda akapata nguvu ya kuendelea kuvaa jezi hiyo ya bluu endapo klabu yake hiyo itafanikiwa kulaza kombe la Europa ndani ya viunga hivyo na jambo hilo pekee linaweza kuwa na nguvu ya kumshawishi japo kwa nafasi fulani. Lakini kinyume na hapo itakuwa na ugumu kwa nyota huyo kuendelea kusalia.

Mbelgiji huyo amekuwa akihusishwa na kujiunga na klabu kubwa ya Madrid kutokana na hali ya mkataba wake unaoenda kuisha 2020 lakini kuna uwezekano mkubwa wa nyota huyo kuondoka kama ukame wa mataji utaendelea kikosini hapo na jambo hilo hadi sasa linakuwa gumu upande wa Chelsea ambao bado wanahitaji huduma ya nyota huyo.

Nyota wa zamani wa klabu hiyo ya Chelsea, Gudjohnson ambaye alitimkia Barcelona 2006 anajua hali halisi ya klabu hizo kubwa kama zikihitaji huduma kutoka kwa mchezaji fulani. Na ana uhakika kwamba kama hali ya hewa ikiendelea hivyo basi kuna kila linalowezekana kwamba nyota huyo akaondoka kutokana pia na hali ya mkataba wake.

Kwa aina ya watu kama Hazard hawahitaji kukaa ndani ya klabu kwa kipindi cha hata miaka mitatu bila kuwa na taji la aina yoyote hivyo nguvu ya kushinda kombe hilo walilopo kwa sasa linaweza kuwa na nguvu zaidi kuwapa ari ya kupambana nyota wengi wakaondoa hofu ya kuendelea kukaa bila kuwa na heshima ya vikombe.

Vijana hao wa Maurizio Sarri wapo katika upande mzuri wa kusonga mbele kwenye michuano hiyo ya Europa jambo ambalo linakuwa changamoto upande wake ni namna wanavyoweza kusonga mbele na aina ya timu zilizopo kwenye hatua hiyo. Klabu hizo zina njaa ya kuchomoka na kikombe hicho muhimu.

Kwa uhalisia Hazard ni mchezaji wa viwango vya juu ambaye haipingiki atawafaa sana Madrid kwa wakati huu na hata kipindi kijacho kutokana na uwezo, kipaji na kasi aliyonayo uwanjani wakati wa kupambania timu yake. Jambo hilo linampa heshima kubwa sana ndani ya klabu hiyo ya Chelsea hivyo wanapaswa kumfanya asalie ndani ya viunga vyao.

Mashabiki wa Chelsea wameanza kupoteza imani yao juu ya kocha wao na aina ya uchezeshaji wa kikosi chake hicho ambacho wengi wanaamini kinajitosheleza kabisa kunyanyua makombe ambayo yapo mbele yao.

2 Komentara

    Uefa lazima waingilie hazard ni mchezaj mkubwa

    Jibu

    Hazard mwamba

    Jibu

Acha ujumbe