Ugarte Kujiunga Man United Jumla sasa

Kiungo wa klabu ya PSG raia wa kimataifa wa Uruguay Manuel Ugarte anatarajiwa kujiunga na klabu ya Manchester United kwa uhamisho wa kudumu kwasasa tofauti na ilivyokua mwanzo.

Taarifa zilieleza awali kabisa klabu ya Manchester United walimuhitaji Ugarte kwa uhamisho wa kudumu lakini kutokana na dau ambalo PSG walikihitaji ikawalazimu Man United kumuhitaji kiungo huyo kwa mkopo baada ya kushindwa dau ambalo lilikua linahitajika na PSG.ugarteManchester United kwasasa wako tayari kumnunua kiungo huyo kwa Euro milioni 60 kama ambavyo PSG walihitaji na hii imerahisishwa na kiungo wa klabu hiyo Scott Mctominay kua mbioni kujiunga na Napoli ya Italia, Huku Man United wakipokea kiasi cha Euro milioni 30.

Manchester United wanatarajia kuongezea kiasi cha Euro milioni 30 kutoka kwenye kiasi cha pesa walichovuna kwa Napoli na kuwapa PSG ili kukamilisha dili la Manuel Ugarte ambaye ameonesha nia ya kujiunga na mashetani wekundu tangu mwanzoni mwa mwezi wa sita.

Acha ujumbe