Katika mfululizo wa zile mechi za kirafiki ambao unaendelea leo itapigwa mechi kali ya kirafiki kati ya mataifa mawili makubwa kimpira ambapo timu ya taifa ya Uingereza itaikaribisha timu ya taifa ya Brazil.
Uingereza ndio watakua wenyeji wa mchezo huo wa kirafiki ambapo watakipiga dhidi ya timu ya taifa ya Brazil, Mchezo ambao unatarajiwa kua mkali sana kwani timu zote zina ubora mkubwa sana.Timu ya taifa ya Brazil chini ya kocha Fernando Diniz imekua kwenye kiwango kizuri kwasasa, Huku vijana wa Gareth Southgate nao wakiwa kwenye utimamu wa hali jambo ambalo linafanya mchezo huu kusubiriwa kwa hamu sana usiku wa leo.
Jude Bellingham, Phil Foden, Harry Kane ni baadhi tu ya majina ambayo yataitumikia Uingereza huku upande wa Brazil wao watakua na wachezaji wao muhimu kama Vinicius Jr, Rodrygo Goes, pamoja kiungo fundi Lucas Paqueta anayekipiga pale Westham United.Timu hizi zimekutana miaka mingi iliyopita kwenye michuano rasmi na hata kwenye mchezo wa kirafiki, Hivo baada ya miaka mingi kutokutana katika mchezo wowote ambapo ilikua ni kiu ya wapenzi wengi wa soka na leo usiku utapigwa mchezo huo.