Leo ndio hitimisho la michuano ya Euro 2024 ambapo utapigwa mchezo wa Fainali katika jiji la Berlin ambapo timu ya taifa ya Uingereza dhidi ya timu ya taifa ya Hispania ambapo kila ttimu itahitaji kuweka historia.
Uingereza wanafanikiwa kuingia fainali ya Euro kwa mara ya pili mfululizo baada ya kufanya hivo mwaka 2021 na kupoteza kwa mikwaju ya penati dhidi ya timu ya taifa ya Italia, Leo watamenyana na kikosi cha timu ya taifa ya Hispania ambao nao wanataka kuweka rekodi ya aina yake.Hispania kwa upande wao wamefanikiwa kutwaa mataji matatu ya Euro mpaka sasa wakiwa sawa na Ujerumani, Hivo leo watahitaji kutengeneza historia mpya kama watafanikiwa kutwaa taji leo kwakua watakua wamefanikiwa kutwaa taji hilo mara nne mara nyingi zaidi ya timu yeyote kwenye historia ya michuano.
Timu ya taifa ya Uingereza hawajawahi kubeba taji la ulaya huku wakiwa wamebeba taji moja kubwa ambalo ni kombe la dunia na imepita miaka mingi, Kwani tangu mwaka 1966 walipotwaa kombe la dunia hawajawahi kubeba taji lingine kubwa na leo ni nafasi kwao kutengeneza historia.Timu ya taifa ya Hispania kuelekea mchezo huu wa fainali ndio timu inayopewa nafasi zaidi kutwaa taji hilo kutokana na kiwango bora walichokionesha mpaka sasa, Timu hiyo chini ya kocha De la Fuentes mpaka sasa wamefanikiwa kushinda michezo yote sita, Hivo wakifanikiwa kubeba taji leo mbele ya vijana wa Southgate watakua wamevunja rekodi yao wenyewe ya mwaka 2008 ya kubeba taji la Euro bila kupoteza mchezo hata mmoja.
This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.
Strictly Necessary Cookies
Strictly Necessary Cookie should be enabled at all times so that we can save your preferences for cookie settings.
If you disable this cookie, we will not be able to save your preferences. This means that every time you visit this website you will need to enable or disable cookies again.