Timu ya taifa ya Uingereza watakwenda kukutana na timu ya taifa ya Italia katika mchezo wa michuano ya Uefa Nations League katika kundi la tatu.

Michuano hiyo inayozihusisha timu kutoka barani ulaya ambayo inaendelea wakati huu ambapo ligi mbalimbali barani ulaya zikiwa zimesimama kupisha michuano hii.

Mchezo huu unaozikutanisha timu hizi mbili bado unaendelea kua mchezo wa kisasi hasa upande wa timu ya taifa ya Uingereza ambao walipoteza fainali ya michuano ya mataifa ya ulaya mwaka 2021 waqlipofungwa kwa mikwaju ya penati na Italia.

uingerezaTimu zimewahi kukutana mwezi juni katika michuano hiihii lakinim mchezo ulimalizika kwa sare ya bila kufungana baina ya timu hizo kitendo kinachofanya mchezo huo kuendelea kua wa kisasi.

Mchezo huu utakwenda kupigwa katika dimba la San Siro nchini Italia ambapo mchezo wa awali uliomalizika kwa suluhu mwezi juni ulipigwa katika dimba la Wembley ambapo timu ya taifa ya Uingereza walikua wenyeji kama ambapo leo Waitaliano watakua wenyeji wakiwakaribisha waingereza.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa