Uingereza Kibaruani Tena Leo Dhidi ya Ubelgiji

Timu ya taifa ya Uingereza chini ya kocha Gareth Southgate leo itashuka tena dimbani katika mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Ubelgiji usiku wa leo.

Mchezo uliopita timu ya taifa ya Uingereza ilikubali kichapo cha bao moja kwa bila dhidi ya timu ya taifa ya Brazil katika dimba lao la nyumbani la Wembley, Huku leo wakiwa nyumbani tena kuwakaribisha Ubelgiji.

UingerezaSouthgate na vijana wake leo watajaribu kuhakikisha wanalinda heshima ya nyumbani baada ya kukubali kichapo katika mchezo uliomalizika dhidi ya mabingwa mara tano wa dunia timu ya taifa ya Brazil.

Katika mchezo wa leo timu ya taifa ya Uingereza inatarajia kua na mshambuliaji wake namba moja na nahodha wa kikosi hicho Harry Kane ambaye alikosekana katika mchezo uliopita dhidi ya Brazil, Ni wazi ataongeza nguvu kikosi hicho kuelekea mchezo wa leo dhidi ya Ubelgiji.

Acha ujumbe