Timu ya taifa ya Uingereza imefanikiwa kumaliza mechi zake katika hatua ya makundi kwenye michuano ya Uefa Nations League na kushika mkia katika makundi kundi la tatu.

Uingereza wameshika mkia katika kundi lao baada ya kucheza mechi ya mwisho jana usiku dhidi ya timu ya taifa ya Ujerumani baada ya kutoka suluhu ya magoli matatu kwa matatu.

Vijana hao wa Garry Southgate wamefanikiwa kucheza sita katika hatua ya makundi kwenye michuano ya Uefa Nations League na kutokushinda mchezo hata mmoja baada ya kusuluhu michezo mitatu na kufungwa michezo mitatu.

uingerezaBaada ya timu hiyo kutoka Ardhi ya mfalme Charles baada ya kumaliza kundi lao bila kushinda mchezo wowote ni rasmi sasa timu hiyo itashuka daraja kuelekea michuano inayofuata Uefa Nations League.

Harry Maguire beki wa timu hiyo pia ameendelea kua gumzo baada ya jana kuendelea kua na kiwango kibovu katika mchezo  na kusababisha moja ya magoli ambayo timu yake iliruhusu siku ya jana.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa