Ujio Mpya wa EPL Msimu Huu

Kama siku zote wasemavyo wahenga ‘Safari ya kesho huandaliwa leo’ basi haya yameanza kujibainisha mapema sana katika ligi kuu ya Uingereza ambayo imeanza marekebisho ya mapema kabisa kwa baadhi ya sheria zake ambazo zilikuwa wakati mwingine zinaleta ugumu kwa waamuzi kutoa maamuzi yao wakati wa kutafsiri sheria husika katika mchezo wanaouchezesha.

Sheria hizo zimeidhinishwa na bodi ya mpira wa miguu ya kimataifa ijulikanayo kama International Football Association Board [IFAB], kwamba kuanzia msimu huu kanuni hizo zitaanza kuwekwa katika matumizi halali. Kutokana na baadhi ya mabadiliko na kanuni inaonekana kabisa kuna baadhi ya klabu zitaumizwa moja kwa moja na mabadiliko hayo.

Miongoni mwa mabadiliko hayo ni juu ya sheria ya mchezaji kushika [kunawa] mpira, awali sheria hii ilikuwa na mapungufu kidogo kwamba ili kutolewa kwa faulo endapo mchezaji ameunawa mpira huo iwepo suala la kuangalia kama alifanya makusudi kuudaka au mpira ulimkuta kwa bahati mbaya. Kuanzia msimu ujao aina hii ya mpira utaanza kuhesabika kama ni adhabu na sio kuangalia tena nia ya aliyekutana na aina hiyo ya mpira kama ilivyo sasa.

Pia, endapo mpira utafungwa au kupita lango kwa msaada wa mkono iwe kwa bahati mbaya au makusudi, basi mpira huo utawekwa kama sehemu ya faulo kutokana na sheria mpya iliyotoka hivi karibuni inampa maamxi mwamuzi kuweza kuurudisha mpira na kucheza kama adhabu kuelekea lango la mpinzani. Mfano goli lililofungwa na Willy Bolly dhidi ya Man City kwa sheria hizi lingezuiliwa.

Pamoja na mabadiliko hayo anaweka wazi kwamba kuunawa mkono itabaki kama sheria lakini haitaendana na yale yalikuwepo nyuma hususani kwa kuangalia kwanza nini lilikuwa lengo la mchezaji wa mpira huo. Hivyo ili kuboresha zaidi wamekuta hakuna haja ya kuendelea kukomalia sheria tata.

Kingine kilichoongezwa katika sheria hiyo ya kuunawa mpira ambayo ilikuwa na walakini sana kimaamuzi ni kwamba endapo mchezaji ataunawa mpira na ukamgusa eneo la chini la umbo lake la mwili basi mpira huo utatolewa kama adhabu kwa timu ya upande wa pili kuprwa upendeleo juu ya hilo.

IFAB pia wanejaribu kuangalia suala la muda unaotumiwa na wachezaji uwanjani katika kufanya mabadiliko hivyo wamefikia maamuzi kwamba ; kutokana na wachezaji kutumia dakika nyingi wanapofanyiwa mabadiliko kuna haja ya mchezaji kutoka nje ya uwanja kupitia maeneo ya upande wa golikipa alipo au pembezoni mwa uwanja alimo, bila kusubiri hadi azunguke afike afike eneo lililo benchi lake la ufundi. Sheria hii ikianza kutumika itawagharimu sana baadhi ya we wanaotegemea nafasi za kutumia pengo hilo kusukuma dakika endapo wameshinda.

Acha ujumbe