Kila mwanasoka ana mapenzi yake na timu fulani kama shabiki, lakini anaweza kuwa na mapenzi na timu nyingine kadhaa kulingana na wakati na kinachomvutia kwenye timu husika. Jurgen klopp amekuwa akizimikia timu kadhaa, ukiacha klabu anayofundisha.

Meneja huyu wa Liverpool  aliwahi kuweka wazi timu zake sita anazozikubali na pia hutumia mda wake mwingi kuziangalia mara kwa mara. Katika timu alizotaja, kati ya hizo mbili ni wapinzani wake wa Ligi Kuu ya Uingereza na mabingwa wengine wa Ulaya.

Klopp alisema hayo wakati Liverpool wakiwa kwenye maandalizi ya kukutana na Barcelona kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa, mzunguko wa kwanza iliyochezwa Mei 1, 2019. Liverpool walichapwa bao 3 bila kwenye mechi hii ya mzunguko wa kwanza.

Jurgen Klopp alisema kuwa Manchester City ni moja ya klabu ambazo anafurahia kuitazama kila wanapocheza na huwa anajifunza kutoka kwao. Hawa ni wapinzani wao wakubwa EPL.

Klabu zingine ambazo klop alitaja kuzikubali ni pamoja na Barcelona aliokuwa anaenda kukutana nao. Tottenham ambao pia ni wapinzani wao wengine wa EPL, Barcelona, Bremen, Dortmund na Mainz.

Meneja huyu Aliamini kuwa alikuwa na kibarua kigumu kupambana na Barcelona, kweli hakukosea, lakini alijipa matumaini kuwa vijana wake hawatalaza damu. Bahati mbaya walichapwa kwenye mechi hiyo ya ugenini. Liverpool walilipa kisasi kwa kumchapa Barca 4-0 kwenye mechi ya mzunguko wa pili, ya Mei 7, 2019 walipokuwa wenyeji.

43 MAONI

  1. Hata kama alikuwa na mapenzi na hizo timu lkn haimaanishi kwamba asipende timu nyingine haya ni mapenzi yake na timu yoyote ile

  2. Klopp anasema ukwel sio kwake tu hata sisi mashabiki huwa tunakuwa na timu pendwa pia tunavutiwa na timu nyingine

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa