Nyota wa Barcelona, Lionel Messi amekuwa mchezaji mwenye mapenzi na klabu ya Barca kwa mda mrefu. Pengine kuliko mchezaji yeyote mwingine wa Barcelona.

Messi amenukuliwa mara kadhaa kuwa hahitaji kuondoka klabuni Barcelona. Ripoti zilitaja kuwepo kwa jitihada za kuhakisha Messi anasaini mkataba wa Kusalia Barca maisha yake yote ya soka. Lakini akanukuliwa akisema ‘hahitaji mkataba wa maisha’ klabuni hapo.

Kama Messi akisaini mkataba wa maisha ina maana kuwa nyota huyu atasalia klabuni hapo hadi kustaafu soka lake. Lakini staaa huyu aliona bado siyo sahihi kwake kujifunga kiasi hicho na kuona huo sio mkataba mzuri kwake licha ya ukweli kuwa anaweza kuwepo hapo maisha yake yote hata bila mkataba wa namna hiyo.

Messi aliweka wazi kuwa Barca walipendekeza asaini mkataba wa maisha, ila yeye aliona si sawa. Mwaka 2019 Akizungumza na Radio Metro Lionel Messi alisema;

“Ni kweli Barcelona walinipendekezea mkataba wa maisha, lakini nilichokisema ni kuwa sitaki mkataba ambao unanifunga mimi kiasi hicho. Nahitaji kuwa sawa kuendelea kucheza, niendelee kupambania magoli hapa. Naweza kuwa hapa maisha yangu yote, lakini bila huo mkataba wa maisha. Naweza kuwepo hapa maisha yote.”

Bila shaka Messi ana ‘Miss” ushindani wa Cristiano Ronaldo, aliwahi sema kuwa ulikuwa unaipa thambani sana debi ya Barca na Real Madrid na pia iliongeza thamani yake kiushindani kwenye ligi ya La Liga.

45 MAONI

  1. Sawa kabisa kukataa mana binadamu huwa mawazo yanabadilika labda ipo Siku ataenda kucheza sehemu nyingine

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa