United na Barcelona Kugongana Vichwa kwa Estupinan

Klabu za Manchester United na Barcelona Zinaripotiwa kuwa zote zipo kwenye mbio za kuwania saini ya Pervis Estupinan kutoka Watford.

United walikuwa wa kwanza kuhusishwa na uhamisho wa beki huyu wa kuhsoto wa Watford kabla ya kubainika kuwa wanakumbana na upinzani mkali kutoka kwa mabingwa wa La Liga, Barcelona na pia Atletico Madrid ambao wanatajwa tajwa.

Beki huyu mwenye miaka 22 alikamilisha usajili wake na Watford mwaka 2016, lakini hakupata nafasi ya kuichezea klabu hiyo. Ametumika zaidi kwa mkopo nje ya Watford na kwa sasa akiwa klabu ya Osasu.

Beki huyu amecheza gemu 27 za La Liga msimu huu na kuonesha uwezo ambao umevivutia vilabu vingi vya Ulaya.

United na Barcelona Kugongana Vichwa kwa Estupinan
SEVILLA, HISPANIA – MACHI 01: Pervis Estupinan (Kulia) wa Osasuna na Jesus Joaquin Fernandez “Suso” wa Sevilla FCwakiwania mpira mechi ya Sevilla FC vs CA Osasuna

Jarida moja la Hispania limnetaja kuwa Man United na Atletico walikuwa wameonesha nia ya kuinasa saini mapema kabisa tangu April. Barcelona nao sasa wameunga tela.

Wakati United ikijitahidi kupanga kutotumia pesa kubwa kwenye usajili, klabu ilituma mawakala wake kumtupia jicho. Ripoti ya mawakala ni kuwa wamependa maajabu yake, wengependa awepo United. Ushindani uliopo unaweza kuwaacha wakaambulia patupu.

 

40 Komentara

    Wazee wa the Red devil changamkieni fursa iyo

    Jibu

    njoo Barcelona Estupinan

    Jibu

    United kwa sasa sidhani kama watamsajili huyu kwani kama wanaupinzani na Barcelona naona Barcelona watakua tayari kutoa dau kubwa kutokana na timu yao ilivyo kwa sasa #meridianbettz

    Jibu

    Kwa man utd utafit kwa mfumo#meridianbettz

    Jibu

    Watagongana vichwa lakini ukweli unajulikana Man U pesa wanayo watampata tu

    Jibu

    Wamsajili tu

    Jibu

    Kwel hapa Barcelona’s inamchikua maana Estupinan mwenyew alishaonyesha mapenz na club hiyo kwa upande mwingine wakala siku zote wanaangalia maslai ya mchezaji na Barcelona inayo tayar dau la kumpata

    Jibu

    Ishu ni mkwanja yeyote atakaye fikia makubaliano na timu husika anaweza kuelekea huko

    Jibu

    Beki hatari sana huyu

    Jibu

    United wamekuwah watu wa romanci tu end of the day deal fail hapo nawapa nafas wazee wa nou camp wanawez kumchukuwah fundiii wa mpr thnks meridian bet kwa update za michezo

    Jibu

    Man united wanachungulia hela kwa sasa naona Barcelona watamchukuwa

    Jibu

    Kurugenzi yetu sijui inafail wapi watumie tactic za movichi tu unaingia mazima tu

    Jibu

    Asante kwa taarifa meeidianbet

    Jibu

    Mwenye pesa nyingi apo ndio atachukua jembe hilo

    Jibu

    😆😆😆😆😆😆 mwenye kisu kikali ndio mlaji wa nyama acha nione itakuaje

    Jibu

    Duh

    Jibu

    Mwenye kisu kikali ndo atakula nyama

    Jibu

    Pesa ndio kila kitu hapo

    Jibu

    Zote ni club kubwa kwa yeyote atakaye weka mzigo wa kutosha anaweza kukamilisha deal

    Jibu

    Zote timi kubwa, mwenye kisu kikali atakula nyama

    Jibu

    Hapo kazi kwake ni vema akaangalia ni wapi panafaa aende

    Jibu

    Habari zote muhimu za michezo tunazipata hapa mpo vizuri#meridianbettz

    Jibu

    Mwenye mawe ndio atafaidka

    Jibu

    Beki mzur huyu

    Jibu

    Ni vizuri Kama atakaa arizike mwenyewe
    Na aangaliye maslai yako wapi

    Jibu

    Beki namkubali sana#meridianbettz

    Jibu

    Ahsante kwa taarifa

    Jibu

    Kila wanapoingia United wanakuta Timu zingine nazo zinawinda hapo hapo#Meridianbettz

    Jibu

    Beki bora

    Jibu

    Waswahili wanasema mwenye kisu kujali ndio atakaekula nyama

    Jibu

    Duuuh

    Jibu

    gud newz asante

    Jibu

    Wakaze Barcelona

    Jibu

    Wamsajili tu

    Jibu

    Inaonekana yupo vizuri mpaka kila mtu anamtaka yy

    Jibu

    Estupinan muda wake umefika kuzitesa club Lusaka saini yake

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    Hizi tetesi za mchezaji kuhitajika na timu hiii ama ile ni mbinu tu za mawakala kwa kushirikiana na vyombo vya habari kuongeza dhamani yao sokoni#meridianbettz

    Jibu

    Yuko vizuri kijana.

    Jibu

    Yupo vizuri

    Jibu

Acha ujumbe