Edwin van der Sar amethibitisha Manchester United na Real Madrid wamevutiwa na Kiungo wa klabu hiyo, Donny van de Beek. Van de Beek amefunga mabao 41 na Assists 34 kws zaidi ya mechi 175 kwa Ajax.

Van de Beek, 23, amekuwa akihusishwa na The Red Devils tangu msimu uliopita alipoisaidia Ajax kwenye mchezo wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa, lakini kuna upinzani wa kumsajili kiungo huyo kutoka Real Madrid.

, United na Madrid Wavutana kwa Donny van de Beek, Meridianbet

Mholanzi huyo amehusishwa sana na kuhamia Real Madrid na inaaminika alifikia makubaliano binafsi na miamba hao wa La Liga kabla ya janga la coronavirus… Lakini, janga hilo limekuwa na athari kubwa ya kifedha kwa mpira wa miguu na Madrid haziwezi kulipa cash kwa Ajax.

Hiyo imefungua mlango kwa United, ambao wamemfuatilia van de Beek kwa miaka miwili iliyopita na ripoti wiki hii zinadai Red Devils ilifungua mazungumzo na Mholanzi huyo juu ya kuhamia Old Trafford.

Van der Sar, kipa wa zamani wa Man United, ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Ajax, alisema: “Ni wazi kwamba vilabu kama Real Madrid na United vinaonyesha kupendezwa na Donny van de Beek”.

50 MAONI

  1. aaah!! anastahili kuwaniwa na vilabu vikubwa kama hivi kwa cv aliyonayo, kokote atakapotua watalamba dumee!!!

  2. Ila me naona mkurugenzi Ana mpigia debe mchezaji wake maana man u Kuna kiungo ambae Ni hulka ya uyo mchezaji Yani uchezaji wao unafanana me ninacho kiona Apo anapigiwa debe

  3. Ni wazi kwamba vilabu kama Real Madrid na United vinaonyesha kupendezwa na Donny van de Beek kweli kizuri kinajiuza kibaya kinajitembeza

  4. Anafanya vizuri sana ndo maana anawaniwa na vilabu vikubwa ,inapendeza sana kijana mdgo akawa na maajabu kama hayo.

  5. Lakini, janga hilo limekuwa na athari kubwa ya kifedha kwa mpira wa miguu atakae weka dau zuri ndo atampata tunabaki na ule usem usemao mwenye kisu kikal ndo mla nyama

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa