Baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Liverpool jana usiku, Manchester United wamerudisha matumaini ya Liverpool kucheza Uefa msimu ujao.

The Red Devils walijikuta wakicheza chini ya kiwango na kufanya makosa kadhaa yaliyowagharimu na kuwapa faida Liverpool. Roberto Firmino alikuwa kwenye wakati mzuri baada ya kupachika magoli mawili akisaidiwa na Jota (goli 1) na Salah (goli 1).

Licha ya Bruno Fernandez na Marcus Rashford kupachika magoli 2 kwa United, pointi 3 muhimu zilikwenda kwa vijana wa Jurgen Klopp.

Ushindi dhidi ya United, unawapandisha Liverpool mpaka nafasi ya 5 wakiwa na tofauti ya pointi 4 (wakiwa na mchezo mmoja pungufu) dhidi ya Chelsea katika nafasi ya 4 na pointi 6 pungufu ya Leicester City katika nafasi ya 3.

United, United Waipandisha Hadhi Liverpool, Matumaini ya Uefa Yaanza Upya., Meridianbet
Roberto Firmino (kushoto) anakuwa mchezaji wa kwanza wa Liverpool kupachika magoli mawili dhidi ya Manchester United kwenye mchezo wa EPL katika uwanja wa Old Trafford. Steven Gerrard alifanya hivyo mwaka 2014.

Vijana wa Ole Gunnar Solskjaer wameambulia vipigo viwili mfululizo ndani ya siku 4 na hii inawapa mashaka mashabiki wa klabu hiyo kuelekea kwenye mchezo wa fainali ya Ligi ya Europa utakaochezwa Mei 26,2021.

Kumkosa Harry Maguire kumekuwa ni moja ya sababu ya ukuta mbovu kwenye kikosi cha Solskjaer na pengine hali ikawa ni hivi hivi kwenye michezo yote ambayo beki huyo atakosekana.

Liverpool wanahitaji pointi zote 9 huku akiombea sare au mmoja kufungwa wakati Leicester City atakapochuana na Chelsea. Kama itatokea hivi, Liverpool atamaliza msimu akiwa kwenye nafasi 4 za juu kwenye msimamo wa EPL msimu huu.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

United, United Waipandisha Hadhi Liverpool, Matumaini ya Uefa Yaanza Upya., Meridianbet

CHEZA HAPA

8 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa