Hatma ya nyota wa Juventus, Cristiano Ronaldo bado imejawa na sintofahamu. Suala la malipo makubwa likitawala habari za uhamisho wake.
Wakala wa Italia Andrea D’Amico anaamini kwamba Cristiano Ronaldo huenda akaondoka Juventus na kujiunga tena na Manchester United wakati wa msimu huu wa usajili wa majira ya joto.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36, kwa mara nyingine alikuwa kwenye fomu bora ya kufunga mabao akiwa na Bibi kizee wa Italia wakati wa msimu wa 2020-21, akiona nyavu mara 36 katika mechi 44 za mashindano yote.

Mustakabali wa Mreno huyu huko Turin unaendelea kutiliwa shaka, ingawa kuna maoni kwamba ana hamu ya kutafuta klabu mpya mwaka mmoja kabla ya kumalizika kwa mkataba wake.

Cristiano Ronaldo

Vyanzo kutoka klabuni Juventus, vimesema kuwa klabu inatarajia Ronaldo kupunguza mshahara wake kwa kuwa hakuna vilabu vinaonekana vipo tayari kumlipa €30m anayolipwa sasa na Juve.

Vilabu kama Paris Saint-Germain, Real Madrid na Man United, pia Inter Miami vinahusishwa kuhitaji huduma ya Staa huyu. Lakini suala la malipo linaendelea kutatiza pande zote ukizingatia madhara ya kiuchumi yaliyosababishwa na COVID-19.

Hata hivyo, D’Amico anasisitiza kuwa Man United ndiyo mahali ambapo Ronaldo anaweza kwenda, akitaja uwezekano wa dili la kubadilishana wachezaji linalomhusu Paul Pogba.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

5 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa