United Watasubiri Kuhangaika na Usajili wa Beki Mpya!

Manchester United wanaripotiwa kuwa hawaoni tena kama wana uhitaji wa kuweka kipaumbele kumleta mlinzi mpya wa kati kwenye dirisha la uhamisho la kiangazi kutokana na fomu ya hivi karibuni ya Harry Maguire.

Beki huyo ghali zaidi ulimwenguni ameisaidia United kupata hati tano safi katika mechi zao tisa za mwisho kwenye mashindano yote.

Maguire United

United waliripotiwa kuwa walikuwa na wasiwasi wa kushuka kwa kiwango cha cha Maguire mwanzoni mwa msimu, bila kusaidiwa na maswala ya nje ya uwanja.

Kwa mujibu wa Manchester Evening News, kurejea kwenye fomu kwa beki huyu mwenye umri wa miaka 27 kumepunguza shinikizo la utaftaji wa mlinzi mwingine kwa Mashetani Wekundu.

Taarifa inasema kuwa United wanaweza kurejea kwenye soko kutafuta walinzi ikiwa Maguire atacheza kwa kiwango cha chini katika siku zijazo, ingawa hiyo inategemea mchango wa Victor Lindelof na Eric Bailly pia kati ya sasa na msimu wa joto.


 

TUNGENEZA FAIDA KUPITIA KASINO YA MERIDIANBET

Neptune’s Richies ni mchezo Unaokupa pesa chap chap huku ukiwa unaburudika kupitia Kasino ya Mtandaoni ndani ya Meridianbet.

Neptune's-Riches_Casino-Post_30-January

Cheza hapa

12 Komentara

    Kwaujumla wanaona Kama washa kaa vizuri

    Jibu

    Wako vizuri kwa sasa

    Jibu

    United wanaendelea kujipanga vyema

    Jibu

    United wako vizuri

    Jibu

    United wachezaji walio nao wanawatosha

    Jibu

    Wamejipanga vinzur

    Jibu

    Maguire anatosha

    Jibu

    Juhudi inahitajika hapa

    Jibu

    Fresh

    Jibu

    Maguire yupo vizuri

    Jibu

    Haina haja tena

    Jibu

    wajipange upya

    Jibu

Acha ujumbe