Klabu ya Manchester United yapoteza mchezo wake wa kwanza wa Europa akiwa nyumbani kwake dhidi ya Real Sociedad ya Hispania kwa bao moja kwa bila . Mchezo huo ulipigwa Old Traford ambapo United waliwaalika Sociedad.

 

United Yaanza Vibaya EUROPA

United walipigwa bao hilo katika kipindi cha pili kwa mkwaju wa Penalty ambapo bao hili ndilo liliifanya Sociedad apate alama tatu za muhimu akiwa ugenini. Ten Hag aliweza kufanya mabadiliko kwenye kikosi chake tofauti na kile kilichocheza dhidi ya Arsenal.

Kwa upande wa Ronaldo inakuwa ni mechi yake ya kwanza kucheza michuano hii ya Europa toka aanze mpira na jana wakapoteza mechi hiyo wakiwa nyumbani ambao sio mwanzo mzuri na Cristiano hakufanikiwa kufunga bao.

 

United Yaanza Vibaya Europa League

Mechi ijayo kwenye Europa vijana wa Ten Hag watacheza dhidi ya Sherrif ambaye katoka kushinda ushindi mnono wa mabao matatu kwa bila, Lakini kabla hawajaenda huko Jumapili watakuwa ugenini kukipoiga dhisi ya vijana wa Partick Vieira Crystal Palace ambao wapo vizuri na wanaleta ushindani kwenye ligi kuu ya Uingereza.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa