Klabu ya Manchester United wanamfuatilia Antoine Griziemann katika kujiandaa na ofa ya mwezi Januari Griziemann mwenye umri wa miaka 31 yupo kwa mkopo katika msimu wa pili ndani ya Atletico Madrid.

 

United Yamtaka Griziemann

Lakini mshindi huyo wa kombe la Dunia la mwaka 2018 la Ufaransa hadi sasa amecheza kama mchezaji wa akiba chini ya Diego Simeone msimu huu huku klabu mbili za Laliga Atletico na Barcelona zikipangiana masharti ya mkataba yake.

Na United nayo itakuwa tayari kuingilia kati kupata mkataba wa kudumu wa mshambuliaji huyo ambapo wakati huo Erick Ten Hag akiendelea kuboresha kikosi hicho. Wanariadha wanadai kuwa Mashetani wekundu hawakufanikiwa msimu huu wa joto na sasa wanafatilia kwa karibu hali hiyo, pamoja na vilabu vingine kadhaa vya ligi kuu.

 

United Yamtaka Griziemann

Ten Hag mpaka sasa ameshinda mechi tano kati ya sita za mwisho za United, na ushindi wa mwisho wa United ni ule wa juzi walipocheza dhidi ya Sherrif ambapo walishinda 2-0. Lakini kocha huyo Mholanzi ana mpango wa kuboresha kikosi hicho katika maeneo ya ushambuliaji ili kuleta changamoto ya ubingwa msimu ujao.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa