Klabu ya Manchester United iliyopo chini ya kocha mkuu Eric Ten Hag imepata ushindi wake wa kwanza katika michuano ya Europa hapo jana dhidi ya Sherrif ya Moldova baada ya kuitandika mabao 2-0.

 

United Yapata Ushindi Wa Kwanza

United walipata ushindi huo wakiwa ugenini huku mabao hayo yakitupiwa nyavuni katika kipindi cha kwanza cha mchezo, Sancho alifunga bao la kwanza katika dakika ya 17 na baadae wakapata bao kupitia kwa Ronaldo ambapo lilikuwa ni kwa mkwaju wa penati dakika ya 39.

Mechi ya kwanza walianza vibaya baada ya kupoteza mchezo wao wa nyumbani dhidi ya Real Sociedad ya Hispania  kwa bao 1-0, na timu hiyo imeendelea kufanya vizuri ambapo imeshinda mchezo wake wa pili mfululizo baada ya kumtandika Omonia Nicosia kwa mabao 2-1 na mpaka sasa ndiye kinara wa kundi hilo baada ya kushinda mechi zake zote mbili.

 

United Yapata Ushindi Wa Kwanza

Mechi inayofuata kwenye michuano hii ya Europa vijana wa Ten Hag watapepetana na Omonia Nicosia ambaye ndiye kibonde wa kundi hili akiwa hajapata ushindi wowote wala alama yoyote.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa