Timu ya taifa ya Ureno ikiongozwa na nahodha wao Cristiano Ronaldo itajitupa uwanjani leo katika mchezo wa kundi la 2 la michuano ya Uefa Nations League.

Ureno wanakwenda kucheza mchezo huo wakitaka kuongoza kundi hilo linaloongozwa na timu ya Taifa ya Hispania waliokusanya alama nane kwenye michezo minne waliyocheza hadi sasa huku Ureno wao wakiwa na alama saba kwenye michezo minne pia hivo wakishinda mchezo huu wanajiweka katika nafasi nzuri ya kuongoza kundi hilo.

urenoVijana hao wa Fernando Santos watakua nyumbani kuwakaribisha Jamhuri ya Czech baada ya kushinda mchezo wa awali dhidi ya timu hiyo kwa mabao mawili kwa bila mwezi juni mwaka huu.

Mchezo huo unatarajiwa kua na ushindani kwani Jamhuri ya Czech bado wana nafasi ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo kwakua mpaka sasa wana alama sita hivo wakishinda mchezo wa leo wanakua na alama saba na wanakaua wamelingana na alama na Ureno.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa