Urusi Kutokuwepo Euro 2024.

Rais wa shirikisho la soka barani ulaya UEFA Aleksander Ceferin ameweka wazi timu ya taifa ya Urusi kutokuwepo kwenye michuano ya Euro 2024.

Rais huyo amesema hayo kuelekea kupangwa kwa droo ya kufuzu michuano hiyo itakayofanyika Frankfurk oktoba 9 na kueleleza nchi hiyo haitakua miongoni mwa nchi 53 zitazokuepo kwenye droo hiyo itakayochezeshwa ili kupata makundi yatayotoa timu zitakozoshiriki michuano hiyo mwaka 2024.

urusiIkumbukwe Urusi ni mwanachama halali wa shirikisho hilo linalosimamia mpira barani ulaya, lakini hali hii imekuja baada ya nchi hiyo kufanya uvamizi wa kijeshi nchini Ukraine na kusababisha madhara makubwa nchini humo.

Kitendo ambacho kimeichukiza dunia kwa jumla na kuionda nchi hiyo katika michuano hiyo kwani inaaminika mchezo huo ni kwajili ya amani na upendo hivo ingekua ngumu kuungana na wanaoharibu amani katika mchezo wa amani.

Hii imekuja baada ya shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA kuwaondoa katika hatua ya mtoano ili kufuzu michuano hiyo baada ya kufanya uvamizi huo nchini Ukraine.

Acha ujumbe