Chama cha soka ncha Urusi wataendelea kuzuia kushiriki michuano yote inayoendeshwa na shirikisho la mpira barani ulaya UEFA baada ya kushindwa kwenye kesi yao kwenye mahakama ya usuruhushi wa michezo {CAS}.
CAS hawakuona umuhimu wa kuweza kupindindua maamuzi yaliyowekwa na dhirikisho hilo huku ikiwa maamuzi yaliotolewa leo na mahakama hiyo yanahusu kwenye ushiriki wa michuano ya UEFA tu, kwa sasa Urusi wamebakiwa na tumaini moja kuhusu maamuzi ya FIFA ambayo hukumu yake bado haijotoka.

Wachezaji wa urusi na timu mbalimbali kutoka nchini humo zimezuiwa kushiriki mashindano yoyote na mashirikisho mbalimbali ya michezo duniani na ulaya, baada ya serikali ya nchi hiyo kuivamia kijeshi nchi ya Ukraine.
Timu ya taifa ya Urusi ilibidi imalize michezo yake ya kufuzu kombe la dunia mwezi huu lakini FIFA wamezipa ushindi timu zote ambazo zilipaswa kucheza na Urusi, huku timu pekee ambayo ilibaki kwenye mashindano ya ulaya Spartak Moscow nayo iliondolewa kwenye mashindano ya Europa League.
SHAOLIN FORTUNES 100 ONJA LADHA YA USHINDI
Maana ya ushindi mkubwa ipo hapa katika mchezo wa SHAOLIN FORTUNES 100 ndani ya kasino maridhawa za meridianbettz. Kwa dau dogo unashinda zaidi, unaweza kucheza mara nyingi uwezavyo huku ukifurahia ladha ya ushindi.



