Usajili: Fununu Zinapamba Moto 2021!

Tukiwa tunahesabu siku chache kabla ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa Januari 1, 2021. Fununu zinaendelea kushika kasi!!!

Fununu za usajili zinasema Arsenal wanapanga kumpeleka Mesut Ozil Juventus kwa mkataba wa miezi 6 huku wakilipa sehemu kubwa ya mshahara wake. Ikumbukwe, Ozil amebakiza mkataba wa miezi 6 kuendelea kuwepo Emirate na alishagoma kuondoka mpaka mkataba wake uishe.

Mesut Ozil

Arsenal watafanikiwa katika hili??

Tariq Lamptey

Arsenal haohao wanaimani watawazidi kete Man City na Bayern Munich kwa kinda anayekuja kwa kasi – Tariq Lamptey anayekipiga katika klabu ya Brighton, Arteta anamuona Lamptey kama mtu sahihi wa kuziba pengo la Bellerin kama beki huyo ataamua kurudi Barcelona.

Phil Foden

Hali sio shwari kule Etihad, za chini ya kapeti kwenye usajili zinasema Phil Foden hafurahishwi na nafasi finyu anayoipata kwenye kikosi cha Pep Guardiola msimu huu. Ikumbukwe matanio ya Foden ni kupata nafasi kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Uingereza kwenye mashindano ya Uero mwakani.

Christian Eriksen

Unaambiwa mcheza kwao hutuzwa, Tottenham kumrudisha Christian Eriksen mwezi Januari ikiwa ni mwaka mmoja tangu atimkie Inter Millan. Endapo usajili huu utafanikiwa, utakuwa na maana yeyote kwa Eriksen na Tottenham??

Declan Rice

David Moyes anaamini Declan Rice anaweza kubakizwa West Ham, Moyes anaamini njia pekee ya kuwaondoa Chelsea kwenye ramani ni kumuongezea mkataba mnono Rice.

David Alaba

The Red Devils – Manchester United wamejiondoa kwenye kinyang’anyiro cha kumuwania David Alaba. Fununu zinasema United wanazingatia zaidi mtonyo mrefu ambao beki huyo atauhitaji ili atue Old Trafford. 

Mauricio Pochettino

Za kunyapianyapia zinatuambia, PSG wamemaliza mchongo wa kumkabidhi Mauricio Pochettino kikosi cha timu hiyo, hii ni baada ya kukamilisha utaratibu wa kumlipa fidia Thomas Tuchel ambaye anatajwa kupokea kitita cha pauni milioni 5.4.

Tuambie unatamani kuona usajili wa mchezaji gani ukifanyika 2021??? 


VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???

SOMA ZAIDI

14 Komentara

    Ngoja tusubiri usajili wa Arsenal kama utafanikiwa!

    Jibu

    Tunasubiri usajili tuone itakavyokuwa

    Jibu

    Tunawangoja kwa hamu

    Jibu

    Yetu macho tusubilie tuone

    Jibu

    Ngoja tuone nani atalamba galasa nani atalamba dume

    Jibu

    Ngoja tuone

    Jibu

    Tunasubilia usajili tu nan atabaki na nan atasepa

    Jibu

    Washabiki tunasubilia

    Jibu

    Haya tupo

    Jibu

    Goodupdate

    Jibu

    Ngoja tuone

    Jibu

    Saf sana

    Jibu

    Jipange sna

    Jibu

    vichwa hatari sana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.