Usajili Ndani ya Siku 7 za Maamuzi.

Zikiwa zimesalia siku 7 tu, dirisha dogo la usajili barani ulaya kufungwa. Baadhi ya timu (na wachezaji) bado zinajitafakari kabla ya kufanya maamuzi.

Kule Old Trafford, Jesse Lingard anasubiri uamuzi wa bodi ya wakurugenzi wa Manchester United. Hii ni baada ya kocha Ole Gunnar Solskjaer kumkubalia ombi lake la kutaka kusajiliwa mwezi huu lakini bado bodi haijapitisha ombi hilo.

West Ham United ndio timu inayotajwa kutaka kumsajili Jesse Lingard, atafanikiwa?

Pale darajani, Billy Gilmour naye anasubiri hatma yake kwenye dirisha hili la usajili. Kocha Frank Lampard haoni kinda huyu akitolewa kwa mkopo mwezi huu lakini mchezaji huyu anahitaji kupata muda wa kucheza zaidi na hivyo kuondoka Chelsea ndani ya siku 7 zilizobaki ni suluhisho sahihi kwake.

Mikel Arteta amepunguza mzigo kwenye kikosi chake baada ya kuwaondoa Mesut Ozil na Sokratis kwenye dirisha hili la usajili. Kuondoka kwa wawili kunatajwa kuwa njia ya mmoja kuingia. Arsenal wanatajwa kuwa mbioni kumshuka Martin Odergaad kutoka Real Madrid.

Licha ya kutua Spurs kwa mkataba wa miezi 18, Gerdson Fernandes hana namba kwenye kikosi cha Mourinho na sasa anahusishwa na klabu ya Torino kule Serie A. Hapa ndio kunautata kidogo, kimsingi inabidi Benfica wakatishe mkataba na Tottenham ili Fernandes arudi Ureno na kisha Torino watamchukua kutoka huko na sio Spurs.

Swali ni kwamba, Torino wataweza kulipa mshahara anaolipwa Fernandes sasa hivi akiwa na Spurs? Vipi Spurs watakubali kulipa sehemu ya mshahara wake ili aende Torino kwani bado anamkataba na Spurs mpaka mwezi May 2021? Siku 7 zitaamua…


MSHINDANI HUSHINDA BWANA!

Anayejaribu hawezi kutoka kapa Meridianbet! Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet inakuhakikishia ushindi mkubwa kila unapojaribu kuingia mchezoni. Washindi hushindana, ingia mchezoni!

Fairy-in-Wonderland_Casino-Post_25-January

CHEZA SASA

16 Komentara

    Jesse Lingard bora asepe tuu Man U hana chake

    Jibu

    Tena wafanye maamuzi ya haraka

    Jibu

    Siku zimeisha klabu nyingi hazijafanya usajili wa maana

    Jibu

    Wafanye maamuzi yaliyo sahii

    Jibu

    Jesse Lingard hana ubora wa kucheza Man U na Billy Gilmour anatakiwa kupewa muda zaidi Chelsea

    Jibu

    Wanatakiwa umakini wa hali ya juu

    Jibu

    Wajitahidi wafanye maamuzi yaliyo sahihi

    Jibu

    Wafanye maamuzi kwausahihi

    Jibu

    Usajili unapasua vichwa

    Jibu

    Mmh

    Jibu

    Duh wanatakiwa wawe makini

    Jibu

    Sa itakuwaje

    Jibu

    Umakini wa Hali ya juu watakiwa.

    Jibu

    Nice update

    Jibu

    Wafanye mamuzi haraka

    Jibu

    Ngoja tuone

    Jibu

Acha ujumbe