Usajili: Samatta Atolewa Macho!

Nyota wa Tanzania ambaye anacheza soka lake la kulipwa nje ya mipaka ya nchi yake amekuwa kwenye kiwango ambacho vilabu vingi vya soka vimependezwa nacho na vinatamani kwa kila namna kuweza kuingia sokoni zaidi kutaka kumsajili nyota huyo ili aweze kuonesha uwezo wake zaidi.

Samatta amekuwa na rekodi ya aina yake ndani ya soka la Tanzania kutokana na mengi ambayo ameweza kuyafanya hadi sasa. Hiyo ikiwa ni pamoja na kuchukua tuzo mbalimbali nje ya mipaka ya nchi yake kwa kutambua mchango wake mkubwa ndani ya soka hususani katika klabu ya Genk anayoichezea kwa sasa.

Mashabiki wa Genk wamekuwa na furaha sana kuwa na nyota huyo ambaye aliweza kurejesha heshima kwao kwa kuwasaidia kunyanyua kombe la ligi kwa msimu uliopita, jambo ambalo liliwapeleka wao kushiriki michiano mikubwa ya klabu bingwa Ulaya. Safari yao msimu uliopita ilikuwa ya furaha sana japo haijaishia hapo hata kwa msimu huu pia.

Kwa sasa wapo katika michuano ya klabu bingwa japo hawajawa na matokeo mazuri lakini bado ni hatua kubwa wameweza kuipiga kwa wakati uliopo. Lakini ni hatua kubwa zaidi kwa Samatta ambaye anakuwa Mtanzania wa kwanza kuweza kushiriki michuano hiyo mikubwa zaidi duniani.

Zaidi ya hilo amekuwa nyota wa kwanza kutoka Tanzania kuweza kufumania nyavu ndani ya Anfield. Aneweza kupata goli lake mbele ya kikosi cha Klopp ambacho kipo kwenye wakati mzuri sana. Ikumbukwe kwenye mechi ya awali aliwafunga lakini goli lake lilizuiliwa; lakini hakuishia hapo akapambana zaidi na ndoto yake ikatimia.

Kwa sasa kumekuwa na taarifa mbalimbali kwamba vilabu vingi vinavyoshiriki ligi kuu ya Uingereza vimeanza kumfuatilia nyota huyo kutaka kumsajili ndani ya ligi hiyo. Klabu zinazomtazama kwa jicho la pekee nyota huyo ni West Ham na Everton zikiwa zinavutiwa sana na huduma yake kwa sasa.

Kwa rekodi zake za nyuma aliweza kuzamisha magoli 25 kwa msimu uliopita ambayo yalikuwa msaada mkubwa sana katika nafasi ya kunyanyua ubingwa wa ligi kwa klabu hiyo ya Genk. Na uwezo wake wa kucheka na nyavu ndio unaompa nafasi ya kutazamwa sana na vilabu vingine nje ya ligi hiyo anayochezea kwa sasa.

2 Komentara

    Habar njema sana 👍

    Jibu

    Gud news

    Jibu

Acha ujumbe