Moja kati ya sajili za bei ghali zaidi kuwahi kufanyika na klabu ya Arsenal ni pamoja na ule wa Pierre-Emerick Aubameyang uliogharimu £56 milioni, usajili mwingine ni ule wa Alexandre Lacazette ambao uliwagharimu Arsenal £47 milioni. Lakini sajili zote hizo mbili, pamoja na zingine zote zilizowahi kufanyika katika historia ya klabu ya Arsenal, hakuna usajili ghali zaidi ya ule wa Nicolas Pepe kutoka Lille ya Ufaransa.

Usajili wa Pepe kutoka Lille uliwagharimu ‘The Gunners’ kitita cha Pauni milioni 72 na kumfanya Pepe kuwa mchezaji ghali zaidi pale Arsenal.

Winga huyo hatari mwenye asili ya Ivory Coast mwenye umri wa miaka 24, alitia saini mkataba wa kutumikia Arsenal kwa miaka mitano ili aweze kuongeza makali ya safu ya ushambuliaji ya Arsenal hasa ikizingatiwa kuwa alionesha kiwango cha kuridhisha pale Lille.

Pepe Akiwa Lille

Nicolas Pepe alionesha kiwango kikubwa sana akiwa na klabu ya Lille inayoshiriki ligi kuu ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1 aliyojiunga nayo mwaka 2017 akitokea Angers.

Msimu wake wa pili tu katika Ligue 1 (2018/19) ulikua wa mafanikio makubwa kwa Pepe kwani alifanikiwa kuifungia Lille jumla ya magoli 35 na kuwa mfungaji bora namba mbili wa ligi hiyo nyuma ya Kylian Mbappe wa PSG.

Mafanikio yake hayo ndiyo yaliyomshawishi mwalimu Unai Emmery wa Arsenal avunje kibubu kumvuta kikosini winha hiyo machachari mwenye asili ya Ivory Coast.

Pepe Akiwa Arsenal

Msimu wa kwanza wa Pepe katika klabu ya Arsenal haujawa wa kuridhisha kabisa. Kiasi walichotoa Arsenal kumsajili Nicolas Pepe hakionekani kurandana na anachokionesha sasa uwanjani.

Katika michezo 24 aliyocheza na Arsenal Pepe amefunga magoli manne tu huku akipiga pasi saba za mabao. Hii haikaribiani hata na nusu ya pesa iliyotolewa na Arsenal kumnasa winga huyo.

Hii InaMaana Gani kwa Mustakabali wa Pepe?

Kwa kuwa huu ndiyo msimu wa kwanza pekee kwa Nicolas Pepe ndani ya klabu ya Arsenal, hatakiwi kukatiwa tamaa. Arsenal wanatakiwa kumpa muda ili kidogo ili aweze kuboresha kiwango chake ili kiendane na thamani halisi ya pesa iliyotolewa katika usajili wake.

Yawezekana kuwa Pepe anashindwa kuonesha kiwango kikubwa sana kutokana na kuwa ni kwa mara ya kwanza anacheza katika ligi yenye presha kubwa na inayotazamwa zaidi duniani ‘EPL’. Presha nyingine kubwa kwa Pepe ni kutokana na ukweli kwamba Arsenal walimfanya kuwa mchezaji wa nne ghali zaidi katika historia ya Ligi ya EPL nyuma ya Paul Pogba, Romelu Lukaku na Virgil Van Dijk.

36 MAONI

  1. Pepe ni mchezaj mwenye dhamani kubwa na mpr mwng miguu mwake shida ni mwaafrika alafu hajapa form kakawalivyo tarajiah wapenzi na mashabik wake Ila kwa mm naona wampe muda tu thnks meridian bet kwa update za michezo na burudani

  2. Msimu wa kwanza wa Pepe katika klabu ya Arsenal haujawa wa kuridhisha kabisa. Kiasi walichotoa Arsenal kumsajili Nicolas Pepe hakionekani kulingana na uwezo wake uwanjani.#meridianbettz

  3. Arsenal haujawa wa kuridhisha kabisa. Kiasi walichotoa Arsenal kumsajili Nicolas Pepe hakionekani kulingana na uwezo wake uwanjan

  4. Mafanikio yake hayo ndiyo yaliyomshawishi mwalimu Unai Emmery wa Arsenal avunje kibubu kumvuta kikosini winha hiyo machachari mwenye asili ya Ivory Coast.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa