Utamu wa El Clasico

Baada ya safari ndefu ya kuisubiri mechi ya wababe wa ligi ya Hispania, Barcelona na Real Madrid hatimaye mechi hiyo inaenda kushuhudiwa huku wawili hao wakiingia uwanjani kulipizana visasi vya kisoka na kuweza kutambua nani mbabe wa msimu huu baada ya Barcelona kuwa na matokeo mazuri kwa wawili hao walipokutana ndani ya msimu huu.

Zidane atakuwa na kibarua kizito cha kuwaaminisha mashabiki wake kwamba kikosi chake kipo imara hata mbele ya michuano mingine ambayo kama klabu wanashiriki kutokana na kuwa na muendelezo mzuri kwenye ligi jambo ambalo pia litatoa majibu ya mechi zijazo za klabu bingwa ambazo pia zina ushindani mkubwa.

Msimu huu una utofauti kidogo kwa sababu ni tofauti na hapo awali ambapo kulikuwa na miamba wawili ambao kila klabu zinapokutana walikuwa wanatupiwa sana macho ya pekee lakini kwa sasa zaidi ni kumuangalia Messi pekee akiwa na kikosi chake na maajabu yake anayokwenda kuyafanya.

Ronaldo na Messi ndiyo waliokuwa wanaangaliwa kwa nafasi kubwa kwenye mechi kama hizi kwa miaka zaidi ya kumi iliyopita. Kwa sasa Messi ndiye aliyesalia na ndiye ambaye anaonekana kuwa na jicho zaidi la kurushiwa kwenye michuano hii ambayo ilipata umaarufu kutokana na mvutano wa kisiasa kati ya pande hizi mbili.

Zaidi ya hayo, pia, ilipata umaarufu kutokana na vita ya usajili ambayo vilabu hivyo vilikuwa vikifanya tangu miaka iliyopita hadi sasa wakiwa bado kwenye vita kama hiyo ya usajili ambapo kila klabu hujitahidi kufanya usajili wa nyota ambaye ana jina tayari klabuni hapo jambo ambalo huchochea zaidi ushindani wao.

Katika mechi ya leo macho yatakuwa kwa nyota ambaye alionekana kama angeweza kutua klabuni hapo na kuziba angalau nafasi ambayo iliweza kuachwa na Ronaldo. Hazard, ambaye alikuwa majeruhi, ana kila linalowezekana kurejea uwanjani akaonesha upekee wake kwenye mechi hiyo.

Kutokuwepo kwa Ronaldo, pia, kumeifanya mechi hiyo kukosa jicho la upekee sana kama ilivyokuwa hapo awali japo katika soka uzuri uliopo nafasi ya baadhi ya watu huwa ni vigumu kuziba lakini ni rahisi kupata mtu anayeweza kufanya vizuri akafikia hatua ya kusahaulisha wengine juu ya nafasi hiyo.

Hadi sasa wawili hao wanalingana alama kwenye jedwali kukiwa na tofauti ya idadi ya magoli pekee hivyo, wana kila linalowezekana kujijenga na kuonesha maajabu juu ya nani apande juu zaidi kwenye jedwali amzidi mwenzake.

Makala iliyopita

4 Komentara

    Ronaldo na messi wako vzr

    Jibu

    Hatari sana

    Jibu

    Ni moto

    Jibu

    Safiii

    Jibu

Acha ujumbe