Utamu Umerudi Tena!

Miaka ya nyuma kidogo katika mchezo wa kabumbu au soka ligi ya huko Italia mambo yalikuwa murua kweli kweli. Yalikuwa matamu si mchezo, kuanzia enzi za Maradona, Baggio, Batistuta hadi wakina Maldini, Inzaghi, Figo, Ronaldo de Lima, Zidane, Nedved hadi mkongwe Pirlo.

Mambo yamebadilika Serie A

Kiufupi Waitaliano walikuwa na ligi bora yenye wachezaji wenye vipaji lukuki. Baadaye mambo yakabadilika kutokana na kashfa ya upangaji matokeo na ulipaji hafifu mishahara. Hii ilitoa mwanya wa kuibuka tena kwa falme za soka hasa Uingereza, Uhispania na Ujerumani.

Ila mambo yamebadilika tena haswa katika msimu wa 2019/2020. Italia au Seria ‘A’ imeleta ushindani wenye tija kwani mpaka sasa hakuna dalili ya ubingwa kwa timu yoyote ile. Hii ni tofauti na misimu nane iliyopita ambayo katika duru hili la pili Juventus angekuwa kawaacha mbali sana wenziye.

“Imbombo ngafu” au ngoma ngumu kwani Lazio na Inter Milan amewapa Juventus upinzani mkali zaidi. Kuna uwezekano bingwa akapishana kwa alama moja au mbili au akapata kwa idadi ya mabao.

Fahamu takwimu za ligi

Waswahili husema utamu wa pipi ni mate yako mwenyewe, ndiyo ni mate yako mwenyewe hata Mauricio Sarri (Masigara) anajua hilo! Kwani imetuletea Lukaku, Alex Sanchez, AshleyYoung hadi Eriksen kutoka katika ligi ya Uingereza. Inter Milan imekuwa tamu ila Lukaku amekuwa mtamu zaidi. Ukirudi kwa Simeone, Inzaghi yeye anamtegemea zaidi Immobile huyu jamaa yeye anafunga, ndiyo kazi yake ana goli 27 mpaka sasa hakuna mshambuliaji yoyote anayemfikia Ulaya nzima.

Magoli na utamu zaidi Serie A

Ukirudi Juventus utakutana na mnyama CR7 Mzungu au Cristiano Ronaldo huyu amekuja na mashabiki wake kutoka Ureno, Uingereza na Uhispania. Kizuri zaidi ni kuwa hawaangushi, anawadhihirishia ubora wake yaani anazeeka na utamu wake kama muwa vile. Haaahaaa, eti Wazungu wanasema, “Age is just a number” umri ni namba tu, miaka 35 ila ni wa moto vibaya.

Utamu haupo kwenye kumtafuta bingwa tu (cretuddo) bali hata kwenye upachikaji wa mabao. Immobile amekuwa kinara akiwa na mabao 27, kiukweli jamaa yeye anatupia tu, hebu piga hesabu kashafunga penati 10 kati ya 11 alizopiga. CR7 Ronaldo akiwa na 21 yeye ni kuganda hewani tu haaa haaa, ndiyo anaganda na anafunga akiwa juu, kipa Sampdoria atawahadithia vizuri.

Nyuma yao yupo Lukaku mwenye 17, jamani Lukaku ana mbio balaa, anafosi na anapiga mashuti, mambo ni moto, mambo ni fire.

Mario Baloteli ni kepteni!

Nisikupe utamu wote mzee! Si unajua maajabu hayaishi, ndiyo hayaishi, njoo umshuhudie Mario Baloteli akiwa na kitambaa mkononi haa haahaa Baloteli amekuwa team captain sijui nidhamu yake ikoje ndani ya Brescia.

27 Komentara

    Ahsanteni meridian bet kwa taarifa

    Jibu

    Ballotell me namuelewa sana

    Jibu

    Maoni:asante kwa taarifa #Meridianbettz

    Jibu

    Ballotel namkubali sana#meridianbettz

    Jibu

    Ballotel anajua mpira

    Jibu

    Balotelli yupo vizuri

    Jibu

    Kiufupi Waitaliano walikuwa na ligi bora yenye wachezaji wenye vipaji lukuki.

    Jibu

    Baloteli fundii

    Jibu

    Baloteli jembee

    Jibu

    Tulisubiri sana bora irudi

    Jibu

    Balloteli yuko vizuri sana

    Jibu

    Ballotel anatisha.

    Jibu

    Brescia kazi wanayo kwa Baloteli

    Jibu

    Ballotel mkorofi lakini yupo vizuri

    Jibu

    Seria a hatarii

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Inapendeza

    Jibu

    Good news 👍

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    Balotelli haitajiki tena #meridianbettz

    Jibu

    good news izo

    Jibu

    Baloteli mzee wa matukio

    Jibu

    utamu umerud tena pia rekodi za wachezaj mbali mbali zitaendelea pi

    Jibu

    utamu umerud tena pia rekodi za wachezaj mbali mbali zitaendelea pia

    Jibu

    Baloteli Yuko poa sana

    Jibu

    Baloteli jembee

    Jibu

    Gud news

    Jibu

Acha ujumbe