Uwanja ulioko katika mji wa kusini-magharibi mwa Senegal, Sedhiou umebadilishwa jina na kuitwa jina la mshambuliaji wa timu hiyo, Sadio Mane baada ya kuisaidia timu yake kutwaa ubingwa wa Afrika kwa mara ya kwanza.

 

mane, Uwanja wa Sedhiou Wapewa Jina la Sadio Mane., Meridianbet

Mshambuliaji huyo wa Liverpool alifunga penalti ya ushindi wakati Simba wa Teranga ilipowafunga Misri kwa mikwaju ya penati 4-2 na kutwaa ushindi wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Mabao yake matatu na pasi mbili murua kwa taifa hilo la Afrika Magharibi yalimpa tuzo ya Mchezaji bora na sasa meya wa Sedhiou, Adboulaye Diop, anasema uwanja wa soka wa eneo hilo utapewa jina la mtoto wao kipenzi.

“Ningependa, kupitia uamuzi huu wa kutoa jina la Sadio Mané kwa uwanja wa Sédhiou, kuelezea utambuzi wa watoto wote wa mkoa huo, kwa mtu anayejulikana kwa utu wake kwa ujumla, Bambali na mji mkuu wake wa kikanda, ambao ni Sédhiou,” alisema Diop, ambaye ni waziri wa utamaduni na mawasiliano wa Senegal, alinukuliwa.

 

“Sadio Mané anastahili heshima hii.”

 

“Mane anapendwa na mamilioni ya watu kufuatia misaada anayotoa katika mji wake wa nyumbani kwa kuahidi pesa za kujenga hospitali na shule, kuchangia ujenzi wa misikiti na kutoa pesa kusaidia mapambano dhidi ya Covid-19.” aliongeza.

Baada ya mafanikio ya timu yake nchini Cameroon, Mane alisema kuisaidia Senegal kushinda Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza ni jambo kubwa zaidi katika maisha yake ya soka.


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa