Kiungo wa klabu ya Real Madrid Federico Valverde ataungana namshambuliaji wa timu hiyo Karim Benzema kuukosa mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya klabu Rb Leipzig.valverdeKiungo Valverde ambae amekua na msimu bora sana mpaka sasa akifunga mabao saba kwenye michuano yote alipata majeraha kwenye mchezo wa jana ambapo Real Madrid walishinda mabao matatu kwa moja dhidi ya Sevilla.

Kiungo huyo anatarajia kuukosa mchezo unaoufuata wa klabu hiyo kutokana na majeraha aliyoyapata katika mchezo dhidi ya Sevilla na kumfanya kuungana na Benzema ambae pia anaugulia maumivu ya misuli iliomfanya kukosekana katika mchezo wa jana.valverdeKiungo Valverde hatakuepo katika mchezo dhidi ya Leipzig kutokana na orodha ya majina ya wachezaji watakaosafiri na timu kuelekea Ujerumani jina lake likikosekana na hivo kuonesha majeraha aliyoyapata yamemuathiri.

Real Madrid watakua namchezo mchezo siku ya jumanne kukamilisha ratiba ya kundi F huku wakiongoza kundi hilo kwa alama 10 na tayari wamefuzu kwa hatua inayofuata.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa