Ruben van Bommel alikuwa mwiba kwa Shakhtar Donetsk, lakini PSV Eindhoven walilazimika kuridhika na sare ya 1-1 katika mchezo wao wa kwanza wa UEFA Champions League kwenye dimba la Philips Stadion.

Shakhtar walitangulia kupitia Gleiker Mendoza katika muda wa nyongeza wa kipindi cha kwanza, kabla Sergino Dest hajaisawazishia PSV katika kipindi cha pili. Licha ya kuutawala mchezo kwa muda mrefu, wenyeji walishindwa kupata bao la ushindi.
Van Bommel alikuwa miongoni mwa wachezaji waliowasumbua zaidi Shakhtar, akikaribia kuipa PSV pointi zote tatu baada ya kupiga shuti hatari lililopita pembeni kidogo. Hata hivyo, PSV walimaliza usiku huo wakigawana pointi na wapinzani wao.

Baada ya mchezo, Van Bommel alikiri kuwa kikosi kilikuwa na maumivu ya kupoteza nafasi ya kushinda, hasa baada ya kuimarika kipindi cha pili. Mshambuliaji huyo pia alisema PSV hawakuwa na kasi ile ya mchezo waliyoonyesha katika ushindi wao wa 3-1 dhidi ya Ajax.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Van Bommel pia alizungumza kuhusu kiwango chake binafsi, akisema amekuwa akitengeneza nafasi mbele ya lango lakini bado hajapata matokeo anayoyataka kwa upande wa mabao.
Wakati huo huo, Van Bommel aligusia tukio lililozua mjadala mkubwa kwenye ushindi wao dhidi ya Ajax, baada ya kugongana angani kwa kasi na Aaron Bouwman. Tukio hilo lilimpeleka beki huyo mchanga hospitalini akiwa na majeraha kwenye mapafu na mifupa ya kifua.

Van Bommel alikiri kuwa alikuwa na makosa na kueleza majuto yake kuhusu tukio hilo, huku akisema amefurahi kuona Bouwman akiendelea vizuri. Hata hivyo, aliwataka mashabiki na wachambuzi kuwa waangalifu kabla ya kutoa hukumu kali dhidi ya wachezaji kupitia mitandao.


