Van De Beek Asingejiunga Man United

Usajili wa Donny Van De Beek bado unaendelea kuzua gumzo kwa baadhi ya wadau wa soka duniani. Hii ni kufuatia na mchezaji huyo kutopewa nafasi ya kuonesha uwezo wake ndani ya kikosi cha Man United.

Mpaka sasa, Van De Beek hajaanza mchezo wowote wa EPL. Amekuwa akisugua benchi kwa mechi za ligi na hata UEFA (dhidi ya PSG). Amecheza michezo ya Carabao Cup pekee.

Kutokana na uwezo wake, wadau wa soka wanadhani hili ni kosa kubwa kwa mchezaji kama Van De Beek kuchagua kujiunga na Man United na kuwekwa benchi kwa muda wote huu.

Gwiji wa soka la uholanzi – Van Basten, amenukuliwa akisema ” Van De Beek hakupaswa kujiunga na Man United”.

“Ni jambo baya sana kwa mchezaji kama Donny kucheza michezo 6 au 7 pekee mwaka huu. Hii sio sawa kabisa.

“Ninajua anapokea pesa nyingi kuliko alivyokuwa akipokea kipindi cha nyuma. Lakini kama mchezaji bora, unapaswa kuwa makini zaidi na kuangalia nafasi ya kucheza kabla hujasaini kujiunga na timu nyingine.

“Donny angesubiri fursa zingine na angesajiliwa na klabu nyingine.” Van Basten ameiambia Ziggo Sport.

Pamoja na kucheza mara chache, Donny anauwiano wa 83.33% wa kupiga pasi sahihi, hii ni takwimu kubwa kuliko Bruno Fernandes na Paul Pogba. Ameshafunga goli 1 mpaka sasa na kutengeneza nafasi kadhaa za magoli.


Tsh.160,000,000 Kushindaniwa!

Tunazungumzia mkwanja wa Tshs.160,000,000! Kupitia Kasino ya Mtandaonii ya Meridianbet unaweza kuwa milionea wakati wowote.

Kamata Mkwanja wako HAPA🤑

23 Komentara

    Van De Beek asuburi tu hawezi jua man United wanafikiria Nini kuhusu yeye

    Jibu

    Hiyo inaitwa kuuwa vipaji vya watu sasa

    Jibu

    Goodupdate

    Jibu

    Asanten kwa habari

    Jibu

    Duu mbona mambo mazito haya

    Jibu

    Asnt kwa taarif meridianbet

    Jibu

    Kocha anamaono yake yeye ndio anayejua kwann anamuweka van de beek benchi mda wote huo bila ya kumchezesha

    Jibu

    Kocha anajua nn anafanya ndiomaana amemuweka benchi

    Jibu

    Sio poa kwa kile alichokifanya kocha

    Jibu

    Jamanii

    Jibu

    Mambo mazito hayo

    Jibu

    Sio poa kwa kile alichokifanya kocha

    Jibu

    Van Beek tokea mwanzo nadhani alijuwa upinzani atakaokumbana nao lakini alikuwa tayari kupambana, Ngoja tuone lakini ni vigumu sana kupata namba ya kudumu ndani ya Red Deviels

    Jibu

    Duuuh kweli nomaaaa

    Jibu

    Gud news

    Jibu

    Hapambane tu united timu kubwa inabid upambane uwez kupata namba kwy kikos cha kwanza

    Jibu

    Ni swala la muda tu

    Jibu

    Duuh noma sana

    Jibu

    Good news

    Jibu

    Asante kwa taarifa murua.

    Jibu

    Ni jambo baya sana kwa mchezaji kama Donny kucheza michezo 6 au 7 pekee mwaka huu. Hii sio sawa kabisa.

    Jibu

    Habari nzito sana

    Jibu

    Van usiwe naharaka dogo kusugua benchi sio kuto pangwa kwenye kikosi nimamuzi yakocha napia unakuwa unausoma mchezo

    Jibu

Acha ujumbe