Kipa wa zamani wa klabu ya Manchester United kwasasa Mkurugenzi mkuu wa klabu ya Ajax ya nchini Uholanzi Edwin Van Der Sar ameweka wazi mustakabali wake ndani ya klabu hiyo baada ya kuulizwa kuhusu kujiunga na Manchester United.

Gwiji huyo wa zamani wa vilabu vya Ajax, Juventus, na Man United amekua akihusishwa na kujiunga na klabu ya Manchester United baada ya klabu hiyo kumleta kocha mpya raia wa Uholanzi klabuni hapo majira ya joto Eric Ten Haag.van der sarKlabu hiyo inaelezwa kufikiria kumchukua Van Der Sar ambae alifanya kazi kwa ukaribu na Ten Haag ndani ya Ajax wakiamini kumleta gwiji huyo kutasaidia kwa kiwango kikubwa ufanisi wa kocha huyo na kuweza kufanya vizuri klabuni hapo.

Mkurugenzi huyo wa Ajax amekua klabuni hapo kwa muda sasa akifanya kazi kwa ukaribu na makocha tofauti tena kwa mafanikio makubwa na kuendeleza utamaduni wa klabu ya Ajax kukuza vipaji kutoka kwenye akademi yao na kuviplekea kwenye timu kubwa.van der sarLakini Gwiji huyo ameweka wazi ametoka kuongeza mkataba na klabu hiyo siku za hivi karibuni na amekua klabuni hapo kwa miaka kumi sasa, Anafurahia maisha ndani ya Ajax huku akisistiza tusubiri kuona kitakachotokea mbeleni.

Klabu ya Man United inatamani kumpata Van Der Sar kwakua ni mtu ambae anaijua klabu hiyo pia amefanya kazi kwa ukaribu na kocha mkuu wa sasa wa klabu hiyo Ten Haag, Hivo ingekua kazi rahisi kwa waholanzi hao kutengeneza kitu bora klabuni hapo kama walivyofanya ndani ya Ajax.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa