Virgil van Dijk anasema kuwa angependa kuona Liverpool ikisajili baadhi ya “wachezaji wapya” katika dirisha la uhamisho la Januari.

Baada ya kufunga bao katika ushindi wa 3-1 wa Liverpool dhidi ya Aston Villa siku ya jana, Van Dijk alidokeza uwezekano wa shughuli ya uhamisho kutoka kwa klabu hiyo ya Merseyside, huku ripoti zikisema huenda hivi karibuni akajiunga Anfield na mchezaji mwenzake wa Uholanzi Cody Gakpo.
The Athletic iliripoti jana kuwa Liverpool wako kwenye mazungumzo ya hali ya juu na PSV kwa mshambuliaji huyo kwa ada ya awali ya pauni milioni 37 (€42m) na ambaye kwasasa ameshatia saini klabuni hapo.
Kocha Jurgen Klopp alisimamia mechi ya kwanza ya ligi ya timu yake nyuma tangu Kombe la Dunia, bado akiwakosa washambuliaji wawili Luis Diaz na Diogo Jota kutokana na majeraha, na hakuna uwezekano wa kurejea hadi Februari mapema zaidi.

Van Dijk amesma; “Tunatumai wachezaji waliojeruhiwa wanaweza kurejea hivi karibuni, na tunatumai tunaweza kuwakaribisha wachezaji wengine wapya kwenye klabu yetu ya soka. Nafikiri ubora huo unakaribishwa kila wakati Liverpool.”
Gakpo amefunga mabao tisa na kutoa asisti 12 katika mechi 14 za Eredivisie msimu huu, ikiwa ni jumla ya tatu kwa idadi kubwa ya mabao (21) baada ya mechi 14 za Eredivisie tangu 1999-00, nyuma ya kocha wake mkuu wa PSV Ruud van Nistelrooy (27 mwaka 1999) na mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Luis Suarez (25 mnamo 2009-10).

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 pia aliifungia Uholanzi mabao matatu kwenye Kombe la Dunia kabla ya kuondolewa kwa mikwaju ya penalti katika robo fainali dhidi ya Argentina, ambao walinyakua taji hilo nchini Qatar.


