Van Dijk Awaponda wanaomsema Lisandro

Beki wa klabu ya Liverpool na timu ya taifa ya Uholanzi Virgil Van Dijk amewaponda wanaosema beki wa klabu ya Manchester United Lisandro Martinez,Beki huyo amewashangaa watu wanaomsema beki kutokana na kimo chake.

Beki Van Dijk anaamini watu wengi wanaoongelea kimo cha beki huyo wanakosea kwasababu licha ya kimo chake lakini anafanya kazi yake vizuri. Beki huyo amezungumza kuhusiana na uwezo ambao aliuonesha beki katika mchezo dhidi yao.

Kumekua na maneno mengi kuhusiana na beki huyo kutokana na kimo chake labda hataweza kuonesha ubora katika ligi kuu ya Uingereza lakini beki huyo ameendelea kuwashangaza watu wengi kutokana na uwezo anaouonesha.Beki Lisandro Martinez ambae amekua ni miongoni mwa wachezaji bora zaidi kwenye kikosi cha Manchester United na mchezaji bora wa timu hiyo kwa mwezi Agosti ameedelea kuwaacha watu midomo wazi kutokana na ubora wake.

Miongoni mwa watu walioponda ujio wa beki huyo kwenye ligi kuu ya Uingereza ni gwiji wa klabu ya Liverpool Jamie Carragher ambae alisema hamuoni beki huyo kama anatosha kwenye ligi hiyo.

Lakini Van Dijk yeye ameshikilia msimamo wako na kuamini kua United wamefanya usajili mzuri kwakua mchezaji huyo anajituma sana,na ana ubora wa hali ya juu na watu wengi wanaoongelea kuhusu kimo wanaongea vitu vya hovyo tu alisema Beki huyo.

aviator

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

Acha ujumbe