Raisi wa Klabu ya Barcelona Joseph Maria Bartomeu amewalaumu waamuzi wasaidizi wa La liga, kwa kuwapendelea Real Madrid tangu Ligi hiyo kurejea.

Baada ya ushindi wa goli moja kwa sifuri mbele ya Athletic Bilbao siku ya jumapili, baada ya Sergio Ramos kufunga penati waliozawadiwa dakika ya 76 kupitia VAR, vijana hao wa Zinedine Zidane wako mbele kwa alama 4 mbele ya Barcelona zikiwa zimebaki mechi 4.

"VAR Inawabeba Madrid." Raisi wa Barcelona.

Refa Jose Gonzalez aliwapatia penati hiyo baada ya kuangalia marudio katika tv ya uwanjani, ambapo Dani Garcia alimchezea madhambi Marcelo.

Sergio Ramos alikuwa mchezaji wa kwanza kwenda kumshawishi refa huyo kurudia kuangalia tukio hilo. Kitende hicho kinamfanya Bartomeu kuamini Real Madrid wanabebwa katika kuelekea Ubingwa.

"VAR Inawabeba Madrid." Raisi wa Barcelona.

 

“Nimeangalia mchezo San Mames angalau mpaka mwisho wa kipindi cha pili.” Alisema Bartomeu baada ya Barcelona kushinda 4-1 dhidi ya Villarreal Jumapili usiku.

“Najiskia vibaya kwasababu tulikua na Ligi bora duniani, lakini  VAR baada ya COVID-19 imekuwa haitendi haki. Imekua ikibadikisha matokeo na kuisaidia timu moja.”

51 MAONI

  1. VAR nikitu chamwisho kwa wahamuzi akinaubishi ukubali ukatae akuna jinsi wahamuzi ndio washahamua

  2. Barcelona wakishinda wao hawabebwi lakini wakishi wenza Wana bebwa Waache kuleta lawama Zama zao zishaishaga

  3. Huu ni mtazamo wake raisi wa Barcelona ila kwa upande mwengine tumeona mambo Kama haya yanatokea endapo timu Fulani inapokua kileleni au nafasi nzuri maneno hua yanaanza kuzuka Mara wanabebwa mfano kamili haya yametokea kwa Liverpool msimu huu na hata kwa huku kwetu ligi ya vodacom vpl yamezuka Kama haya kua simba anabebwa na hata tukirudi nyuma kipindi kile cha sir Alex furguson kocha was man u maneno Kama haya yalikuwepo kwa sababu tu man ilikua inafanya vizuri kwaiyo tunaweza sema haya ni maneno ya wapinzani kwenye soka au dalili za kushindwa mbio haiwezekani VAR ikawa inapendelea tu time moja ya Madrid.

  4. Maisha hawajawahi kuwa sawa siku zote. Barcelona wameshapoteana na mwisho watamutupia virago Kocha. VAR haijawa msaada kwa refa hasa Ligi EPL#meridianbettz

  5. Hyo ni dalili ya kushindwa kwa Barcelona leo wenzao wana bebwa na VAR wao hawabebwi washaona kombe sio lao tena wanaanza visingizio washaona hakuna wa kutupia lawama zao zaid ya real Madrid na VAR kiukweli tuu Barcelona msimu huu wamepoteana na wana wazee wengi sana pale kalibia kikosi kizima mizee mitupu naVAR n muamuzi wa mwisho.maana kuna matukio mengine ya uwanjan si refa wa ndan ya uwanja au raz men hawawezi kuona matukio nyeti zaid ya hii teknolojia mpya hii ya sasa maana hata ukizid kidole utaonekana tuu kwa hii haina upendeleo

  6. Anachosema var ni kweli Madrid wamebebwa Sana kwny mechi dhidi ya attletico hvy sheria na kanuni za mpira zifate mkondo wake

  7. VAR ni kipimo cha mwisho ndo maana kwa sasa wanakitumia ili kuondoa utata ,kusema hawa wamependelewa au wameonewa

  8. hivi kwann ambapo mechi ikitoke mtu kafungwa kwa gori la kufanyia mtu madhambi.. na ikitokea adhabu watu upenda kulahumu VAR Kama tais wa Barcelona anavyo lalamika.. Kama sikosei hata kocha wa Tottenham Joseph mordhno nae aliwai kulala Mika ila hi yote utokana na mabadiliko na matarajio ya mchezo..

  9. Barcelona hana la kujitetea VAR haibebi timu kinachotakiwa barca ashinde mechi zote zilizobaki ili awe bingwa laliga

  10. Maoni:Duuh hatari kumbe hata VAR haiamini kama iko sahihi, Joseph maria ajipange tu na timu yake asifikilie habari za kubebwa

  11. Ni mtazamo wake kusema hivyo kwa VAR mana hata tunaonaga kwenye mechi nyingine kuwa haitendi haki na upande mwengine inatenda haki haswa kwa kipondi chichi cha kutafuta mabigwa ndio changamoto zake hutokea na kufanya upendeleo usiokuwa na haki

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa